tiko
tiko
MSANII wa
filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake
zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana
huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja
la Brown hakuweza kupatikana ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo
huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa ingawa picha iliyowekwa mtandaoni
ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo ni mpenzi
wake wa siku nyingi.
“Hizo picha ni sehemu ya vipande vya
kwenye wimbo wa huyo mwanaume, ukweli ni mpenzi wangu wa siku nyingi na
anataka kunioa, ndiyo maana kafikia hatua ya kujichora jina langu, sina
kipingamizi, tunaomba Mungu atufanikishe tufunge ndoa,” alisema.
tiko
tiko
Post a Comment