tiko
tiko
Mwanaume
mmoja nchini Brazil ameushangaza umma wa watu baada ya kutembea masaa
mawili kuelekea hospitali akiwa na kisu kichwani baada ya kuvamiwa na
majambazi akitokea klabu.
Kisu hicho ambacho kinadaiwa kilizama kichwani
kwa urefu wa 30cm kilimpata mwanaume huyo kwa jina la Juacelo Nunes
pembeni ya jicho la kushoto na kutokea kwenye shavu lake wakati
akipambana na majambazi hao.
“Kisu kilipita katika baadhi ya mishipa yake ya damu ambayo ingeweza kumuua kutokana na kuvuja kwa damu nyingi,”alisema daktari Gilberto Albuquerque aliyemuhudumia kutoka hospitali ya Teresina alikofikia.
Kisu hicho kilitolewa na kupewa polisi ambao wanaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa daktari alisema mgonjwa huyo kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari na hali yake inaendelea vizuri.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu
wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na
facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment