Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

ALA PASAKA KWA KICHAPO AKIDAIWA KUWA MWIZI!

Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Anton, Jumapili ya Pasaka alikula sikukuu kwa kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kwa madai kuwa ni kibaka.Tukio hilo lililotokea saa 12 asubuhi maeneo ya Sinza Afrikasana ambapo walioshuhudia tukio hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa, kijana huyo aliyefahamika mtaani hapo kama muokota chupa, ilidaiwa kuwa  alikurupushwa kutoka katika nyumba moja ambako alienda kwa gia ya kuokota chupa, akataka kukwapua kitu.


 Anton akivuja damu baada ya kupewa kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kwa kosa la wizi.
 “Baada ya kukurupushwa katika nyumba hiyo, kijana huyo alitoka mkuku mpaka katika nyumba moja ambako alimkuta dada mmoja akifagia na kuingia ndani ya geti  kisha kujifungia,” alisema shuhuda mmoja.

Baada ya muda wakatokea watu waliomkurupusha ndipo dada huyo akawaambia kuwa mtuhumiwa wao ameingia ndani baada kulikuta geti hilo wazi wakati akifanya usafi na alikuwa amejifungia kwa ndani.
Habari hiyo iliwafanya baadhi ya vijana kudandia geti ili kuingia ndani, hata hivyo, kijana huyo alipoona watu hao wakiruka getini naye akaruka ukuta upande wa pili na kukimbia.Akipakizwa kwenye gari safari kuelekea kituoni.
 Lakini juhudi zake hizo za kutaka kutoroka hazikuzaa matunda kwani alidakwa hatua chache kutoka kwenye ukuta wa ua wa nyumba hiyo na kuanza kula kichapo kikali ambacho kilisababisha kuchanwa kichwani na damu nyingi ‘kumwagika.’
 Kijana huyo aliokolewa na askari polisi waliokuwa doria wakiongozwa na Kamanda Rashidi wa Kituo cha Polisi Mabatini waliokuwa katika gari yao ya doria.

Moja ya jeraha kubwa alolipata kichwani baada ya kichapo.
Kamanda huyo na askari wenzake walifanya kazi kubwa kuzuia raia wasilete madhara zaidi kwa kijana huyo huku wakiwaambia wananchi kuwa siyo busara kujichukulia sheria mkononi, walimkamata wakampeleka kituoni kwa hatua zaidi.

Hali tete jijini dar..!! Polisi Yazuia Wafuasi Wa Askofu Gwajima.....Vikosi vya Mbwa, Farasi,Magari sasa kila Kona.


Jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  limesema  wafuasi  wa  Askofu  mkuu  wa  kanisa  la  ufufuo  na  uzima,Josephat  Gwajima  wasithubutu  kutia  mguu  eneo  atakalohojiwa  askofu  huyo.

Kauli  ya  jeshi  hilo  imekuja  siku  chache  baada  ya  Askofu  Gwajima  kuwataka  wafuasi  wake  kumsindikiza  leo  kituo  cha  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  ambako  anahitajika  ili  kuhojiwa.

 Msimamo huo  ulitolewa  jana  na  kamishna  wa  polisi  katika  kanda  hiyo, Suleiman  Kova  wakati  akizungumza  na  mtandao  huu  ambapo  alisisitiza  kuwa  anayehitajika  kufika  katika  kituo  hicho  ni  Gwajima  na  mwanasheria  wake.

Kamishna  Kova  alisema  ni  vema  wafuasi  hao  wakaendelea  na  kazi  zao  za  uzalishaji,kwani  kwenda  kituoni  hapo  bila  mwito  au  kukamatwa  ni  kosa.

Kova  alisema  eneo  hilo  haliruhusiwi  watu  kukusanyika, hivyo  kwa  usalama  wao ni  vyema  wakaendelea  na  shughuli  zao  na  kuliacha  jeshi  hilo  lifanye  mahojiano  na  Askofu huyo  wakiwa  huru.

"Napenda  kutumia  nafuasi  hii  kumuomba  Gwajima  awaambie  wafuasi  wake  hawahitajiki  kufika  eneo  hilo  kwani  anayehitajika  ni  yeye  na  mwanasheria  wake," alisema  Kova.

Kova  alisema  iwapo  kila  mtu  atafuata  taratibu  hakuna  nguvu  itakayotumika  kutoka  jeshi  la  polisi, lakini  endapo  watakiuka  hakuna  njia  mbadala  ambayo  inaweza  kutumika  zaidi  ya  kutumia  nguvu.

Kauli  ya  Kova  inakuja   kutokana  na  kauli  ya  Gwajima  aliyoitoa  wakati  wa  sikukuu  ya  pasaka  kuwataka  wafuasi  wake  kujitokeza  katika  kituo  hicho  wakati  atakapokwenda  kuhojiwa.

Gwajima  alisema  lengo  la  kuwataka  wafuasi  hao  kujitokeza  ni  ili  waweze  kujua  kila  kitu  kinachoendelea  katika  sakata  hilo  kwani  kuna  taarifa  ambazo  zimekuwa  zikizushwa  na  watu  kupitia  mitandao  mbalimbali.

Akizungumzia  hali  ya  usalama  katika  jiji  la  Dar, Kova  alisema  ni  shwari  na  kuahidi  kuwa  wanaendelea  na  oparesheni  ya  kukamata  wauza  dawa  za  kulevya, wahalifu  na  kulinda  maeneo  ya  fukwe.

Pia, alisema  wamejipanga  kukabiliana  na  vitendo  vya  kigaidi  ambapo  wanafanya  uchunguzi  kila  mahali  kwa  kutumia  vikosi  vya  mbwa, farasi,helkopta, magari, pikipiki  na  kutembea  kwa  miguu  katika  maeneo  yote  ya  jiji.

AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUGUNDULIKA KUHUSIKA NA KIFO CHA MAREHEM

Picha  Ya  Maktaba

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
 
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
 
Diwani wa Kata hiyo amesema alipata taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote kukimbiwa baada ya tukio hilo.
 
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.

Yemen:Houthi yavamia mji wa Aden

Wapiganaji Yemen wanakamia Aden
Wapiganaji waasi nchini Yemen wamezidisha mapigano yao katika hatua za kuuthibiti kabisa mji wa Aden.
Nyumba kadhaa zimechomwa moto huku sauti zikisikika kutoka kwenye vipaza sauti misikitini,
ya kuwataka raia wote wa mji huo kujitokeza ili kutetea mji wao usitwaliwe na waasi.
Wakati huo huo, kuna ripoti kuwaege za muungano zikiongozwa na majeshi ya Saudi Arabia zinazounga mkono
Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano
serikali ya Yemen, yakirusha mabomu katika ngome ya waasi katika viunga vya mji wa Aden upande wa kazkazini.
Awali Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano, yanayoongozwa na Saudi Arabia,
katika makabiliano dhidi ya kundi la waasi wa Kishia la Houthi, nchini Yemen.
Awali hali ya taharuki ilitanda kote katika mji huo wa pwani baada ya
Iran imezua taharuki baada ya kutuma Manuari yake katika bahari ya Yemen
Iran Kutuma manuari mbili za kivita katika bahari inayopakana na eneo la Aden nchini Yemen.
Kamanda mmoja wa jeshi la Iran amesema manuwari hizo zimetumwa katika eneo hilo kulinda taifa lake kutokana na uharamia.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa hatua hiyo huenda ikachochea uhasama zaidi katika eneo hilo.
Saudi Arabia inaongoza jeshi la muungano linalokabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa kishia nchini Yemen, wapiganaji ambao wanakisiwa kupewa misaada na utawala wa Tehran.

Ester Kiama: Nammeneji Tu Dude Wala Si Mchepuko Wake

Ester Kiama: Nammeneji Tu Dude Wala Si Mchepuko Wake
Baada minong’ono kuzagaa kila kona kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi kati ya mwigizaji wa kike Ester Kiama na muongozaji na mwigizaji Kulwa Kikumba, mwanadada huyo amekanusha na kudai kuwa yeye ni meneja tu wa msanii huyo na anamsimamia kurudisha Bongo Dar es salaam.
Kweli nipo karibu sana na Dude kikazi na si kimapenzi kama wengine wanavyofikiria, nammeneji tu katika uwezeshaji wa kurudisha kipindi chake cha Bongo Dar es Salaam na masuala ya filamu, tumerekodi sinema yangu ya Ngoma ngumu,”anasema Ester.
Akizungumza na FC  Dude naye aliungana na mwanadada huyo kuwa ni meneja wake na wana malengo ya kufanya makubwa naye hawezi kufanya ujinga huo kwani ana familia yake anayoiheshimu na hawezi kumsaliti mkewe Eva anampenda sana, na masuala ya kazi tu, hakuna mapenzi.
“Ester kwa sasa ni meneja wangu wala sina uhusiano naye nipo naye kikazi na ndio meneja wangu kwa sasa katika kazi zangu za kisanaa katika filamu na Bongo Dar es Salaam,”anasema Dude.
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top