tiko
tiko
Kijana
mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Anton, Jumapili ya Pasaka alikula
sikukuu kwa kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kwa madai kuwa ni
kibaka.Tukio hilo lililotokea saa 12 asubuhi maeneo ya Sinza Afrikasana
ambapo walioshuhudia tukio hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa, kijana
huyo aliyefahamika mtaani hapo kama muokota chupa, ilidaiwa kuwa
alikurupushwa kutoka katika nyumba moja ambako alienda kwa gia ya
kuokota chupa, akataka kukwapua kitu.
Anton akivuja damu baada ya kupewa kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kwa kosa la wizi.
“Baada
ya kukurupushwa katika nyumba hiyo, kijana huyo alitoka mkuku mpaka
katika nyumba moja ambako alimkuta dada mmoja akifagia na kuingia ndani
ya geti kisha kujifungia,” alisema shuhuda mmoja.
Baada
ya muda wakatokea watu waliomkurupusha ndipo dada huyo akawaambia kuwa
mtuhumiwa wao ameingia ndani baada kulikuta geti hilo wazi wakati
akifanya usafi na alikuwa amejifungia kwa ndani.
Habari hiyo iliwafanya baadhi ya vijana kudandia geti ili kuingia ndani, hata hivyo, kijana huyo alipoona watu hao wakiruka getini naye akaruka ukuta upande wa pili na kukimbia.Akipakizwa kwenye gari safari kuelekea kituoni.
Lakini
juhudi zake hizo za kutaka kutoroka hazikuzaa matunda kwani alidakwa
hatua chache kutoka kwenye ukuta wa ua wa nyumba hiyo na kuanza kula
kichapo kikali ambacho kilisababisha kuchanwa kichwani na damu nyingi
‘kumwagika.’Habari hiyo iliwafanya baadhi ya vijana kudandia geti ili kuingia ndani, hata hivyo, kijana huyo alipoona watu hao wakiruka getini naye akaruka ukuta upande wa pili na kukimbia.Akipakizwa kwenye gari safari kuelekea kituoni.
Kijana huyo aliokolewa na askari polisi waliokuwa doria wakiongozwa na Kamanda Rashidi wa Kituo cha Polisi Mabatini waliokuwa katika gari yao ya doria.
Kamanda huyo na askari wenzake walifanya kazi kubwa kuzuia raia wasilete madhara zaidi kwa kijana huyo huku wakiwaambia wananchi kuwa siyo busara kujichukulia sheria mkononi, walimkamata wakampeleka kituoni kwa hatua zaidi.
tiko
tiko
Post a Comment