tiko
tiko
SIRI ni moja ni kuwa kama Real Madrid
inahitaji kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu basi inatakiwa kuhakikisha
haipotezi mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Barcelona kwenye
Uwanja wa Camp Nou.
Takwimu
zinaonyesha kuwa mechi za miaka ya hivi karibuni baina ya timu hizo
ambayo inajulikana kwa jina la El Clásico, huwa inakuwa na faida kwa
Madrid kama inashinda kwenye uwanja huo unaomilikiwa na Barcelona.
Real Madrid imetwaa ubingwa katika misimu minne ya 2011-12, 2007-08, 2006-07 na 2002-03 ambayo haikufungwa uwanjani hapo.
Wakati takwimu zikieleza hivyo kikosi
cha Madrid kinachoongozwa na Kocha Carlo Ancelotti kinaonekana kutotulia
huku vita ya wachezaji mastaa ikidaiwa kuigawa timu hiyo, wakati
wenzao, Barcelona wanaonekana kutulia huku makali ya Lionel Messi
yakiongezeka.
Madrid imekuwa na mwendo wa kusuasua
tangu kuanza kwa mwaka huu na inadaiwa kuwa mastaa wake, Cristiano
Ronaldo na Gareth Bale hawana uhusiano mzuri.
Upande wa Messi ameongeza kasi ya
kufunga mabao ambapo miezi miwili iliyopita alikuwa amezidiwa mabao 12
ya kufunga na Ronaldo, lakini mpaka sasa Messi anaongoza katika ufungaji
akiwa na mabao 32 huku Ronaldo akiwa na 30.
Akizungumzia mechi hiyo, Luis Suárez wa
Barcelona anasema yupo tayari kwa ajili ya mchezo huo kwa kuwa anajua
historia na umuhimu wake ni mkubwa.
“Nakumbuka ule ushindi wa mabao 5-0 (wa
Barcelona), nilikuwepo uwanjani siku hiyo, niliona mambo mengi jinsi
watu walivyoshangilia lilikuwa jambo zuri na la kipekee,” alisema
Suarez.
Aidha, kurejea uwanjani kwa kiungo, Luka
Modric kunadaiwa kuamsha morali ya Bale ambaye hakuwa kwenye kiwango
kizuri kwa muda. Modric alikuwa nje kwa muda mrefu, katika mechi
iliyopita alicheza na Bale akafunga mabao mawili, wawili hao walicheza
pamoja Spurs kabla ya kutua Madrid.
tiko
tiko
Post a Comment