tiko
tiko
Taarifa
ya kuokolewa kwa watoto 80 katika kambi ya kundi la Boko Haram huko
Cameroon imedaiwa kwa sasa hawawezi kukumbuka tena majina yao kwa mujibu
wa afisa aliyewatembelea.
Watoto hao wenye umri wa miaka 5 hadi 18 hawawezi kuzungumza lugha yoyote ile kulingana na maelezo ya Christopher Fomunyoh,ambaye ni mkurugenzi wa kitaifa wa taasisi ya National Democratic Institute {NDI}.
Watoto hao walipatikana katika kambi Kaskazini mwa Cameroon mnamo mwezi Novemba mwaka jana.
Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria
limepanua mashambulizi yake hadi nchini Cameroon na wapiganaji hao
wanajaribu kusimamisha taifa lenye uongozi wa kiislamu kaskazini
mashariki mwa Nigeria.
Hivi karibuni kundi hilo liliahidi kuiga mfano wa kundi la Islamic State ambalo limeteka eneo kubwa la Syria na Iraq.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia
mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram
na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment