tiko
tiko
Najua umenisubiri kwa hamu kubwa bi
shosti, ni mimi yuleyule mtambo wa kurekebisha tabia nimeingia kama
upepo wa kimbunga. Kwa vile nia ya kona hii ni kutibu si kubembeleza
watu wala kuangalia sura zao. Unajua kuna baadhi ya wanawake wanatia
kichefuchefu kufanya utani katika ndoa na kuzifanya ndoa za siku hizi
zipoteze maana na kushindwa kutofautisha yupi kaolewa na yupi kahaba.
Nimebahatika kuhudhuria kicheni pati
nyingi nikiwa kama mgeni mwalikwa, nashukuru Mungu kila aliyenialika
alikubali ushauri wangu. Siku zote nimekuwa nikiwaeleza kuwa anayejua
ladha ya kitu ni yule aliyekionja hata akikielezea atakielezea kwa
ufasaha zaidi tofauti na yule asiyeijua ladha atabahatisha kwa vile
alisikia tu muonjaji akielezea utamu na uchungu wa kitu kile.
Kwa kweli bado nalia na maadili mabaya
katika ndoa za watoto wetu wa karne hii, wewe mzazi unaalika watu kuja
kumfunda mwari wakiwa hawajui nini maana ya ndoa kwa vile wamesikia basi
ndiyo wanatoa mafundisho kwamba ndoa inatakiwa hiki na hiki, kwa
kukisikia na si kwa uhalisia ndiyo maana wanakaa uchi mbele ya mwari
sasa wamekuja kumfundisha mema au maovu?
Leo nataka kuzungumza na kina mama
wakosa haya wasiyojua vibaya, inawezekana kabisa ndoa yako inawaka moto
kutokana na ujinga wako kiburi kujisikia humjali mume unataka kila kitu
ukipate usipopata mumeo humpi haki ya ndoa. Leo hii wewe unamcheza
mwanao na kuwaita wakosa haya wenzako mje mumfunde mwari.
Mtamfundisha nini kama siyo wewe kuwa
chanzo cha kuiharibu ndoa ya mwanao? Hao mashoga zako wanatoa nasaha za
aibu mbele ya binti yako anayetaka kuolewa nawe upo pembeni unapiga
vigelegele mtoto kaolewa kesho kaachika mbaya nani?
Japokuwa kicheni pati si sehemu sahihi
ya kumfunda mwari, basi tutafute watu waliodumu kwenye ndoa zao kwa muda
mrefu ili waweze kutoa nasaha halisia wala si za kuhisia. Hata mavazi
yao ni somo tosha kwa mwanao kuonesha mwanamke anatakiwa kustiri maungo
yake kwa vile mhusika wa kuyaona ni mumewe tu.
Mbele unamsimamisha mwanamke mwenye sifa ya kuchanganya wanaume kama zege nguo alizovaa mwili wote upo nje na yeye anakueleza eti ndoa ni ngumu mheshimu mumeo. Wakati yeye pengine ameachika ndoa zaidi ya tatu.
Mbele unamsimamisha mwanamke mwenye sifa ya kuchanganya wanaume kama zege nguo alizovaa mwili wote upo nje na yeye anakueleza eti ndoa ni ngumu mheshimu mumeo. Wakati yeye pengine ameachika ndoa zaidi ya tatu.
Siku zote mfano mzuri ni wa vitendo si
wa maneno, anayekufunda ukimuangalia kweli anachokisema ndicho
anachokifanya. Kwako unamchukulia kama mfano wako katika maisha ya ndoa,
ili ukiteleza basi umkimbilie mara moja kukupa mungozo wa ndoa yako
ili ujue umejikwaa wapi na ufanye nini.
Kingine wazazi sisi ndiyo tunatakiwa
kuwa viongozi wa watoto wetu waipende ndoa kupitia maisha yetu ya ndani
ya wewe na mumeo. Ndani ya nyumba hamzungumzi au mama anamdharau baba.
Pale unamfundisha nini mwanao ina maana na yeye atajua kumbe kumdharau
mwanaume ni jambo la kawaida na ni haki ya msingi.
Kama kweli tuna nia nzuri na watoto wetu
basi sisi ndiyo walimu wa kwanza kuhakikisha ndoa zao zinadumu.
Tujiepushe kuwashirikisha watu wasiojua thamani ya ndoa, kila aliyeionja
ndoa ataielezea kwa ufasaha zaidi ili muolewaji basi apate faida na
kujiandaa vizuri katika ndoa yake.
Wazo langu jipya ambalo najua
litakushtua lakini kama wazazi mtalifanya hili basi nina imani watoto
wenu wa kike watapata faida kubwa katika ndoa zao.
Muda ukikaribia mtoto wako wa kike
kuolewa kama hakupitia unyago mweke chini ukiwa na shoga zako waliodumu
kwenye ndoa zao kwa muda mrefu mwelezeni ndoa ni nini, utamu na uchungu
wa ndoa ambao wote umebebwa na upendo, heshima, adabu, huruma na
uvumilivu.
Nina imani somo hili likifanyiwa kazi, tutafanya ndoa zipate heshima kuliko kuwaita wahuni kutukana mbele yamwari wetu. Yangu leo yanatosha tukutane wiki ijayo.
Nina imani somo hili likifanyiwa kazi, tutafanya ndoa zipate heshima kuliko kuwaita wahuni kutukana mbele yamwari wetu. Yangu leo yanatosha tukutane wiki ijayo.
tiko
tiko

Post a Comment