tiko
tiko
DIVA wa
miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, juzikati alijikuta
akilewa chakali kiasi cha kushindwa kupanda boti iliyokuwa imeandaliwa
maalum kwa ajili ya kwenda kusherehekea tukio la kukatwa keki katika
kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya msanii mwenzake, Estelina Sanga
‘Linah’, iliyofanyika Slipway, Masaki jijini Dar.
Shilole alikuwa amealikwa kwenye sherehe hiyo iliyoanza kurindima jioni
ya saa 10 ndani ya Ukumbi wa Paparazi, ambapo waalikwa walianza kupata
mapochopocho zikiwemo pombe na baadaye kutakiwa kupanda boti ili kwenda
kumalizia sherehe katikati ya maji kwa kukata keki.
Kutokana na kubugia kiburudisho kupita kiasi, Shilole alishindwa kupanda
boti iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa bahari na hivyo kumpa kazi ya
ziada mchumba wake Nuh Mziwanda aliyelazimika kumrudisha garini ili
warejee nyumbani.
“Kusema kweli mimi hata sielewi nilishindwaje kupanda boti, network
ilikata, nilishangaa tu kujikuta nipo kwenye bethidei ya Menina
Mikocheni, nafikiri kilichotokea muulize baby wangu Nuh Mziwanda,”
alisema Shilole baada ya kuulizwa kuhusu ‘kuzimika’ kwake.
Nuh Mziwanda alikiri kuwa mpenzi wake alipoteza fahamu, kiasi cha
kumlazimisha yeye kumbeba na kumrudisha tena klabu ya Paparazi ambako
alipatiwa maji baridi kwa wingi huku akipigwa na kiyoyozi cha nguvu
kabla ya kwenda kwenye shughuli ya Menina
tiko
tiko
Post a Comment