tiko
tiko
KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amewatoa wasiwasi mashabiki wa
timu yake na kusema kuwa ana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa
leo dhidi ya Mgambo, ingawa amekiri utakuwa mgumu kutokana na hali ya
hewa na mazingira ya uwanja.
Yanga ambayo imeweka kambi katika Hoteli
ya Capital City, leo inatarajiwa kuwa mgeni wa Mgambo JKT kwenye Uwanja
wa Mkwakwani.Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, alisema
hana hofu na mchezo huo licha ya timu yake kutokuwa na rekodi nzuri
uwanjani hapo, alisisitiza anachotaka kupata ni pointi tatu na
kusisitiza kuwa mpira hauchezwi kwa historia.
“Michezo ya mikaoni mara nyingi ni
migumu kutokana na mzingira jinsi yalivyo, mfano huu uwanja una maji
lakini tunatakiwa kupambana na kupata pointi tatu.“Mgambo ni timu nzuri,
lakini mchezo wa soka hauchezwi kwa historia, timu iliyojiandaa vizuri
na kutumia nafasi ndiyo itakayoshinda katika mchezo husika.”
Msimu uliopita, timu hizo zilipokutana
katika Uwanja wa Mkwakwani, Yanga ililala mabao 2-1 jambo linaloongeza
ugumu wa mchezo huo.Mabao hayo yote mawili yalifungwa na waliopeleka
kilio kwa Simba, Malimi Basungu na Fully Maganga ambaye alisababisha
penalti iliyopelekea Msimbazi kulala bao la pili Jumatano iliyopita.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment