tiko
tiko
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nuh
Mziwanda, ametoa kali ya mwaka kwa kudai kwamba kitendo cha kupigwa mara
kwa mara na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kinampa furaha na
ufahamu wa namna anavyopendwa.
“Kwanza kupigwa raha, mpenzi wako
asipokupiga hakuonei wivu, mimi nafurahi sana na namtaka anipige tu!
kila siku akijisikia, ananidhihirishia kuwa ananipenda,” alisema.
Nuh alisema mengi yamesemwa kutokana na
kupigwa kwake mara kwa mara, huku akidai kwamba hilo halina tatizo
kwake, kwa kuwa halitaharibu mapenzi yao wanayoamini yatafika mbali.
“Sisi tunawezana na Mungu atusaidie tufikie katika hatua ya ndoa tuliyojiwekea,’’ alimaliza.
tiko
tiko
Post a Comment