tiko
tiko
MWANAMKE mmoja mkazi wa Gongo la Mboto
jijini Dar es Salaam, Violet Manyondo (40) anadaiwa kumtesa na kumfanyia
vitendo vya kikatili mtoto wake wa kumzaa, anayejulikana kwa jina la
David (14).David ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule
moja ya msingi iliyopo Mzambarauni, Dar kwa sasa haendi shule kutokana
na majereha aliyonayo kiasi cha kuwaliza majirani.
Akizungumza na Amani, mmoja wa majirani
aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ni mara yake ya kwanza
kushuhudia mama akimtesa mtoto wake wa kumzaa kama anavyofanya mama
huyo.“Tunaomba vyombo vya haki za binadamu hata Jeshi la Polisi
kushughulikia tukio hili haraka iwezekanavyo vinginevyo mtoto huyo
ataathirika kisaikolojia, halafu cha kushangaza, ana watoto watatu,
lakini ni huyu tu ndiye anayekutana na kipigo,” alisema jirani huyo.
Alisema katika kumsaidia kijana huyo,
wamewahi kwenda kituo cha polisi Gongo la Mboto, lakini polisi jamii
walipokwenda nyumbani hapo, waliambulia matusi.Mtoto David aliliambia
gazeti hili kuwa ni kweli mama yake anamtesa kwa muda mrefu na kwamba
hivi karibuni alikwenda kumshtaki katika kanisa lao liitwalo Universal
Ufalme wa Mungu, Mzambarauni, Ilala, Dar na alipotakiwa kumwita mama
yake alikataa kwenda.
“Baada ya mama kupata wito ule hata
kanisani ameacha kwenda kwa kuhofia kikao na ushauri wa viongozi wa
kanisa. Sina cha kufanya wala pa kwenda, namuomba Mungu anisaidie
nimalize shule,” alisema kijana huyo.
Kuhusu sababu za kuteswa, alisema hafahamu chochote, ingawa alihisi huenda ni kwa sababu ya baba yake kutopeleka hela ya matumizi nyumbani, kitu ambacho hata hivyo haifahamu kwani hamfahamu mzazi wake, zaidi ya kusikia kuwa ni dereva wa daladala.

Katika hali ya kushangaza, mama huyo alipotafutwa na gazeti hili, alijibu kijeuri;
“Yule ni mwanangu, naweza kumfanya lolote lile. Mimi ni mzazi wake, natakiwa kumrekebisha kwa njia yoyote.” Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto umesema unashukuru kwa kupata taarifa hizo, kwani watahakikisha wanafuatilia jambo hilo na kulipatia ufumbuzi.

Kamanda Msangi: “Ni kweli tukio hilo
limetokea na inadaiwa kuwa chanzo cha kifo cha mtu huyo ni kipigo
kilichotokana na imani za kishirikina.”
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment