Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUUU CHA ST.JOSEPH AKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA MILIONI 10/-‏

tiko tiko
Meneja wa NMB tawi la Benki House jijini Dar es Salaam, Leon Ngowi (kushoto) akipanga kitita cha shilingi Milioni 10/- wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita hicho Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim (kulia) aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, katikati ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu. Hafla hiyo ilifanyika  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kushoto)akimkabidhi kitita cha shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim (kulia) aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na kampuni hiyo.Katikati ni  Meneja Uhusiano wa NMB Vicent Mnyanyika. Hafla hiyo ilifanyika tawi la NMB House  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Mshindi wa kitita cha shilingi  Milioni 10/- kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Ibrahim M. Ibrahim ambaye ni Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph tawi la Songea (kulia)akiowaonesha kitita chake waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitita hicho na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia katikati ni Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB Vicent Mnyanyika. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandshindi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kumkabidhi cha shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(katikati)aliyejishindia kupitia Promosheni ya JayMillions  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni  Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB,Vicent Mnyanyika. Hafla hiyo ilifanyika  katika tawi la NMB benki house jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Jay Millions”(kushoto) akimpongeza kwa ushindi wa shilingi Milioni 10/- Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha ST. Joseph, Ibrahim M. Ibrahim(kulia)alizojishindia kupitia promosheni hiyo na kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu(hayupo pichani)wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika tawi la NMB benki house jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUUU CHA ST.JOSEPH AKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA MILIONI 10/-‏
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha St.Joseph cha jijini Dar es Salaam, Ibrahim.M.Ibrahim anayesomea fani ya uhandisi wa kusindika vyakula katika kampasi ya Songea leo amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 10/-alizojishindia kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania katika hafla iliyofanyika katika tawi la NMB benki house Jijini Dar es Salaam.
Ibrahim Ibrahim alikabidhiwa fedha zake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu pamoja na Meneja Uhusiano wa NMB Bw. Vicent Mnyanyika mbele ya waandishi wa habari.
Akiongea muda mfupi baada ya kupokea fedha zake za ushindi Ibrahim alisema kuwa siku ya leo itabaki kwenye kumbumbukumbu za historia kwa kuwa ndoto yake ya kusoma shahada ya pili muda mfupi baada ya kuhitimu masomo ya shahada ya kwanza imetimia .“Vodacom kupitia promosheni hii wamefanya ndoto yangu ya kuwa mhandisi msomi kutimia kwa kutumia shilingi mia tatu tu na kuandika neno  JAY kwenda namba 15544”.Alisema Ibrahim kwa furaha.
"Promosheni ya Jaymillions imelenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini na washindi wengi waliopatikana hadi sasa wametoka kwenye makundi ya watu katika jamii wanaohitaji kuwezeshwa kimaisha ili wajikwamue na kuinua hali zao kama vile  wajasiriamali wadogo wadogo , wamachinga, mama ntilie,wanafunzi na wazee wastaafu.
Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa ameishapatikana mshindi mmoja wa milioni 100/-,Washindi wanne wa Milioni 10 na washindi 38 wa Milioni 1/-
Mshindi wa milioni 100/- ni Uwezo Madengenya kutoka  Wilayani Kilolo mkoani Iringa.  Washindi wa milioni 10/-  ni – Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa , James Mangu (Mwanza),Zuena Rajabu (22) anayefanya kazi ya ususi mkazi wa Tabata Segerea na Deborah Stanley (23) ambaye naye pia  ni msusi na mkazi Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhisiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyo ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kujiendeleza kielimu.
Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao  za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.
Kwa upande wake Meneja wa Uhusiano wa benki ya NMB, Vicent Mnyanyika alimpongeza  mshindi na kumshauri kuweka akiba ya fedha hizo benki ili kuhakikisha zinakuwa salama hadi utakapofikia muda wa kutaka kuzitumia kutimiza ndoto yake pia alimwakikishia mshindi huyo kuwa benki yao ipo tayari kwa kumpatia mafunzo yaliyo bora ya jinsi ya kuwekeza ili fedha zake ziweze kuongezeka zaidi ya hizo alizojishindia.Pia aliipongeza Vodacom kwa kubuni promosheni za aina hii zenye mwelekeo chanya wa kuinua maisha ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top