tiko
tiko
Utata umegubika uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi baada ya Serikali kutaka kuwasilisha ‘kinyemela’ muswada wa uanzishwaji wa Mahakama hiyo, kwenye Mkutano huu wa 19 wa Bunge unaondelea mjini Dodoma bila kuupitisha kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kama utaratibu unavyotaka.
Pamoja
na utata huo, kwa mujibu wa ratiba ya Bunge iliyotolewa jana, muswada
huo utawasilishwa kwenye kikao cha mwisho cha Mkutano huu Aprili Mosi,
saa chache kabla ya hotuba ya Waziri Mkuu ya kuahirishwa kwa Bunge.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo ya Bunge, muswada huo utawasilishwa Jumatano ya
Aprili Mosi, mwaka huu baada ya kipindi cha maswali na majibu na
umewekwa kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali
(Na. 2) wa mwaka 2014.
Alipoulizwa
ikiwa muswada huo utapata nafasi ya kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema kwa kifupi: "Muulize Katibu wa Bunge, mimi sipangi ratiba ya Bunge."
Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, hakupatikana kwa maelezo kuwa yuko nje ya ofisi kikazi.
Alipoulizwa
kuhusu msimamo wa Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambao
wanapinga kuwasilishwa kwa muswada huo, alisema hawezi kuzungumzia jambo
hilo.
Naye
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu, Samuel
Sitta, alisema kura ya maoni iko pale pale na kwamba msimamo wa Maaskofu
‘hauna’ nguvu kwa kuwa nao wamegawanyika kwa maelezo kuwa wapo
wanaounga mkono kura ya maoni na wapo wanaopinga.
Alisema
viongozi hao wa dini wanapaswa kuwaacha wananchi waamue wenyewe kuhusu
Katiba inayopendekezwa hivyo suala la Mahakama ya Kadhi na Kura ya
Maoni, linapaswa kuamuliwa na Watanzania wote.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, Jasson Rweikiza,
amesema kuwa kamati yake haijapokea muswada huo na kuupitia.
Akizungumza
na gazeti la Nipashe jana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu
Lissu, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala,
alisema inashangaza serikali kutaka kuuwasilisha muswada huo bungeni
kinyemela bila kuuwasilisha kwenye Kamati.
Alisema
awali kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, Kamati ilipokea maoni ya wadau
mbalimbali, zikiwamo taasisi za Kiislamu na viongozi wa dini za
Kikristo, ambao walionyesha kasoro nyingi kwenye muswada na hivyo Kamati
iliiagiza serikali ikafanye marekebisho na kuyawasilisha kwake kabla ya
kupeleka bungeni.
“Sisi
(Kamati), ndiyo wenye muswada na tulikuwa hatujakubaliana, tukawaambia
serikali tupate kwanza maridhiano ya jambo hili kwa sababu tulipokea
maoni ya wadau wengi ambao walibaini makosa na kasoro za kitaalam;
serikali ikaahidi kuyafanyia kazi lakini hadi leo hawajarudi kwenye
kamati kutuletea marekebisho, sasa tunashangaa wameuweka kwenye ratiba
ya Bunge,” alisema.
Alisema
ni hatari kwa mambo yanayoweza kuligawa taifa kama uanzishwaji wa
Mahakama ya Kadhi na Katiba inayopendekezwa kufanywa kwa hila na ubabe
na kuishauri serikali ihakikishe wananchi wameelewa kwa kina jambo hilo
ili kuepuka mgawanyiko usio wa lazima.
Hata
hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya Ofisi za Bunge, zinaeleza
kuwa muswada huo unaweza kusomwa kwa mara ya pili ukiwa sehemu ya
Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa mwaka 2014.
Chanzo
chetu kilieleza kuwa hata hivyo, kuwasilishwa kwa Muswada wa Mhakama ya
Kadhi kutategemea makubaliano kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusiana na mambo gani
yawasilishwe.
Utata
huo umeibuka takribani mwezi mmoja baada ya Serikali kuuchomoa muswada
huo bungeni kwenye Mkutano wa 18 wa Bunge iliofanyika Februari, kwa nia
ya kutafuta maridhiano kwanza.
Aidha,
taasisi 11 za Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ziliazimia
kuwahamasisha wana jumuiya wake kususia Kura ya Maoni ya Katiba Mpya
hadi watakapopata uhakika wa kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye meno.
Baada
ya serikali kuuchomoa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilikutana
Dodoma na serikali iliomba muda wa kufanya maridhiano kabla ya
kuwasilishwa muswada huo kwenye Bunge hili.
tiko
tiko
Post a Comment