tiko
tiko
Mfanyakazi wa ndani, Joseph Matonya (26) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwanagati mwenye umri wa miaka 14.
Akisoma
hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu John Msafiri
alisema kuwa mshitakiwa huyo atatumikia adhabu ya viboko ambavyo
atachapwa sita akiingia na sita akitoka.
Pia alisema Matonya atatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.
Hakimu
Msafiri alisema mshtakiwa alitiwa hatiani baada ya upande wa mashitaka
kuthibitisha mashitaka yake bila ya kuacha shaka kwa kuwa na mashahidi
wanne na PF3 iliyothibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda alidai kwamba mshtakiwa apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Kabla
ya hukumu, mshitakiwa huyo alidai kuwa yeye ni mgeni wa Mahakama na
kwamba familia yake inamtegemea na kudai kuwa hakumbaka mtoto huyo.
Pia alidai kuwa adhabu hiyo imemuathiri kisaikolojia na kimwili na kwamba hatasahau maishani mwake.
Ilidaiwa
kati ya Novemba na Desemba, 2013, maeneo ya Kitunda Mwanagati, wilayani
Ilala, Matonya alimbaka mtoto wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwanagati.
tiko
tiko
Post a Comment