tiko
tiko
Wizara ya ulinzi nchini Marekani imethibitisha kwamba imemuua mojawapo
ya viongozi wa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab kupitia
kombora.
Adan Garaar alituhumiwa kupanga shambulio katika jumba la kibiashara la West Gate nchini Kenya miaka miwili iliyopita.
Maafisa nchini Marekani wanasema aliuawa kusini mwa Somalia ijumaa iliyopita.
Marekani imekuwa ikikagua operesheni hiyo kabla ya kuthibitisha kwamba Garaar ndiye aliyekuwa akilengwa.
Nchi hiyo imewalenga viongozi wengine wakuu katika kundi hilo la
wapiganaji wenye itikadi kali za kiislamu kwa mkombora akiwemo kiongozi
wa zamani wa kundi hilo, Ahmed Godane.
CHANZO: BBC SWAHILI
tiko
tiko
Post a Comment