BINTI aliyefahamika
kwa jina moja la Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu, hivi karibuni
alimtoroka bwana’ke na kuonekana akijiachia hovyo na wanaume watano
tofauti katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam
kulipokuwa na onyesho la Bendi ya Taarabu ya Mashauzi Classic.
Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu akisakata ngoma.
Akionekana
kuwa ‘vizuri’ kichwani, kwa kiburudisho alichopata usiku mnene, binti
huyo alionyesha umahiri mkubwa wa kukata mauno kiasi cha kuwavutia
wanaume ambao kila mmoja alitaka kuwa naye karibu kiasi cha kumfanya
kuwa bize kwa kila wimbo kulazimika kucheza na wanaume tofauti.
Baadhi
ya wanawake waliokuwa na waume zao jukwaani, walionyesha kukasirishwa
na mwenzao huyo, kwani licha ya kuwa hodari wa kucheza, pia aliwaruhusu
wanaume kumkumbatia kadiri walivyopenda, kiasi cha kusababisha wakware
wengi kuwa na hamu ya kushiriki naye.
Hata
hivyo baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo walisema mrembo huyo alitia
aibu kwani kuna wakati alicheza hadi nguo zake za ndani zikawa
zinaonekana.
“Hii
ni aibu jamani, mke wa mtu kucheza namna hii mbaya zaidi hadi nguo
inamvuka yeye hata habari hana,” alisema mmoja wa mashabiki.Hadi
mwandishi wetu anaondoka eneo hilo, mrembo huyo alikuwa akiendelea
kufanya mavituz yake jukwaani.
Post a Comment