tiko
tiko
MTANGAZAJI maarufu
Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa
‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake
aliyefahamika kwa jina la Diana.
Kwa
mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini
wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo
na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa.
“Diana
kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi
ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho
kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu,
alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,”
kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua
anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo
alikanusha madai hayo.
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny
tiko
tiko
Post a Comment