tiko
tiko

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema vyama vya upinzani vitaendelea kuwa wasindikizaji wa CCM katika chaguzi mbalimbali zitakaofanyika nchini kutokana na wananchi wengi kuendelea kukiamini chama hicho.
Aidha
amesisitiza kuwa Katiba Inayopendekezwa itapita kwa kishindo wakati wa
Kura ya Maoni itakayofanyika Aprili 30, mwaka huu, pamoja na kelele na
shinikizo la vyama vya upinzani kutaka wananchi kususia upigaji kura wa
Katiba hiyo.
Nape
aliyasema hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chamwino, wakati
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipofanya ziara wilayani humo
katika mwendelezo wa ziara yake ya kuutembelea Mkoa wa Dodoma.
Akizungumzia
ushindi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa udiwani, ubunge na
urais, Nape alisema hakuna siri kuwa vyama vya upinzani vitaendelea
kuisindikiza CCM ili kushinda viti vingi vya udiwani, ubunge na kushinda
kwa kishindo kwenye uchaguzi wa urais.
“Ndugu
zangu nataka niwaeleze wazi kwamba vyama vya upinzani ni kama mpambe wa
Bwana Harusi, ambaye pamoja na kufanya shughuli zote za usaidizi na
upambe kwa Bwana Harusi lakini safari yake huishia sebule maharusi
wanapofika nyumbani,” alisema Nape.
Alisema
tayari ishara ya ushindi wa CCM imeonekana katika uchaguzi wa serikali
za mitaa, ambapo CCM imeshinda kwa kishindo kwa kunyakua viti vingi
kwenye vitongoji, mitaa na vijiji, huku vyama vya upinzani vikiambulia
ushindi katika baadhi ya maeneo.
“Nataka
niwaambie wazi, wananchi wa nchi hii bado wana imani kubwa na CCM,
ukiona kuna mtu anakipenda chama cha upinzani ujue anasumbuliwa na
ushamba tu na si kitu kingine. Sisi tumezunguka nchi nzima na tumegundua
wakati CCM inazidi kuimarika na kupanda juu, vyama vya upinzani
vinazorota na kushuka chini, wenye macho na walione hili,” alisena Nape.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment