tiko
tiko
SIRI
imefichuka na sasa kila kitu hadharani juu ya kiungo wa Simba, Jonas
Mkude kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Kuna mambo mawili makubwa yaliyotajwa juu ya Mkude kuwekwa pembeni, moja
kubwa ni kuwa utovu wa nidhamu ndiyo kikwazo na Kocha wa Stars, Martin
Nooij hana mpango wa kumuita tena labda abadilike baadaye.
Licha ya kuwa kwenye kiwango kizuri ikiwemo kuwa chaguo la kwanza katika
kikosi cha Simba, Mkude hajaitwa katika kikosi cha Stars ambacho
kitaingia kambini keshokutwa Jumapili kujiandaa kucheza mechi ya
kirafiki dhidi ya Malawi, Machi 29, 2015.
Mtu wa karibu na Mkude ameliambia Championi Ijumaa kuwa
kuna vitu vingi ambavyo Mkude amekuwa akifanya vinamkera kocha huyo na
alichoamua sasa ni kutomjumuisha kikosini kwake na kama akiendelea
hivyo, basi ndiyo inawezekana asirejee tena kikosini hapo mpaka
atakapoondoka.
“Mkude ni mchezaji mzuri lakini kuna vitu anatakiwa kubadilika, hasa
kuzingatia muda. Mara nyingi anachelewa mazoezi akiwa Stars, kitu
ambacho Nooij anakitafsri kama utovu wa nidhamu na kuna vitu vingi vya
chinichini ambavyo amekuwa akifanya havimfurahishi kocha,” alisema mtoa
taarifa huyo.
Sababu ya pili ambayo imetajwa pia kuwa inaweza kuwa imechangia kutoitwa kikosini hapo ni katika masuala ya posho.
“Siyo kwamba kiwango chake kimeshuka ila kuna fitina imefanyika kwa kuwa
zile posho za siku wanazopewa wachezaji wakiwa Stars kuna watu wanataka
‘pasu’. Sasa Mkude huwa anagoma kutoa, ndiyo maana imekuwa nongwa,
wakaamua wamuundie zengwe,” kilisema chanzo kingine cha uhakika.
Gazeti hili lilipozungumza na Mkude juu ya madai hayo, alisema:
“Mwanangu mimi sitaki kuzungumza chochote kuhusiana na Taifa Stars,
mwalimu ameshachagua kikosi chake ambacho ni sahihi, acha waendelee.”
Baada ya kusema hivyo, Mkude hakutaka tena kuulizwa swali linalohusu Stars.
Championi Ijumaa likamtafuta
Meneja wa Taifa Stars, Clemence Boniface ambaye naye alifunguka:
“Ninashukuru kunitafuta kuliongelea hilo lakini hayo mambo hayapo, ni
uzushi tu wa kutaka kutuchafua.
“Wachezaji wakiwa kambini kwa siku wanapewa shilingi 50,000 timu ikiwa
Tanzania, ikiwa nje ya nchi posho ni dola 50 na hakuna mchezaji
anayekatwa.”
Alipotafutwa Nooij na kuulizwa juu ya madai hayo, alisema: “Siwezi
nikalizungumzia suala hilo kwa sasa, nitatoa ufafanuzi siku chache kabla
ya kucheza na Malawi.” Viungo walioitwa Stars ni; Amri Kiemba, Haruna
Chanongo, Frank Domayo, Mcha Khamisi, Salum Abubakari ‘Sure Boy’,
Hassani Dilunga na Said Ndemla.
Wakati huohuo,
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, juzi aligeuka mbogo mara baada ya
timu yake kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mgambo, ambapo
kwanza aligoma kuzungumza na waandishi kisha kupiga teke chupa za maji.
Tukio hilo lilitokea baada ya mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
ambapo baada ya hapo alienda kwenye basi la timu yake na kuanza kupiga
tairi na mlango kwa hasira kisha kuingia ndani huku wachezaji wake
wakiwa kimya.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment