tiko
tiko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Jeshi la Polisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amelitaka
Jeshi la Polisi nchini Tanzania kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na
vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura,
upigaji Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akifunga mafunzo ya maofisa warakibu wasaidizi katika Chuo cha Taaluma
ya Polisi, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema dalili zinaonyesha
kwamba kuna watu wenye nia ya kuhatarisha amani katika matukio hayo.
Alisema Serikali itahakikisha kazi ya uandikishaji katika daftari la
wapigakura, upigaji wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu vinafanyika kwa
amani na utulivu kwa gharama zozote.
Akikuzungumza katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema kama serikali
inatambua changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi hasa katika majukumu
yake ya kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zake, lakini kazi nzito
ikiwa ni wakati huu ambapo Taifa linaelekea kwenye upigaji wa kura ya
maoni kuhusu katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa Madiwani,
Wabunge na Raisi hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kutotumia 'maguvu' ili
kuifanya amani iendelee kutawala katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Aidha Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba Akizungumzia ya Rais
Kikwete, alisema, “Rais Kikwete yeye ndiye mtu wa kwanza kuivuruga amani
kwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa kura ya maoni wakati siyo jukumu
lake na jukumu hilo ni la Tume ya Taifa ya Uchaguzi "NEC" na serikali
yake kushindwa kuratibu vyema mchakato wa uandikishaji.
Profesa Lipumba amesema, na hapa tunamnukuu: "Kama uandikishaji hauendi
vizuri mpaka sasa, anavunja sheria za nchi, halafu yeye mwenyewe tena
anakwenda kwenye vyombo vya dola na kuvieleza vijiandae, wakati yeye
huyohuyo ndiye ameanzisha uvunjifu wa amani tunashindwa tumueleweje,”
mwisho wa kunukuu.
CHANZO: IRAN SWAHILI
PICHA NA MTANDAO
tiko
tiko
Post a Comment