tiko
tiko
PEPO la ugomvi linazidi kumuandama staa
wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’, baada ya kusakwa na jeshi la
polisi kwa kosa la kumjeruhi mtu mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii
huyo ametengeneza kicha cha habari kwa mara nyingine akidaiwa kumpiga
meneja wake aliyefahamika kwa jina la Tall Mnyama.
Katika tukio la awali, TID alidaiwa
kutembeza kichapo na kumjeruhi James Richard, mkazi wa Jiji la Dar kwa
kosa alilodai kuwa ni kupaki gari kwenye eneo lake, maeneo ya nyumbani
kwa msanii huyo, Kinondoni-Sterio jijini Dar.
Tukio la kumpiga meneja wake, TID
anadaiwa kulifanya katika Hotel ya Element, Oysterbay ambapo inaelezwa
kuwa msanii huyo alifika hotelini hapo akiwa na wapambe wake na
alipomkuta meneja huyo, alibishana naye kwa muda mfupi kisha kumzaba
kibao.
“Alimkuta mwenzake (Tall) kaka sehemu,
akamsemesha na alipojibu tu akamzaba kofi, lakini huyu meneja wake
alikuwa mstaarabu, hakumlipizia. Baada ya tukio hilo TID alitokomea na
kama unavyojua sasa hivi anaishi kama digidigi, mbaya zaidi watu
wanasema asipompiga mtu hasikii raha,” kilidai chanzo chetu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’
kuwa, meneja huyo baada ya kupokea kipigo hicho, alikwenda kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Oysterbay kilicho chini ya Camillius Wambura
(pichani) ambapo lilifunguliwa jarada lililosomeka;
OB/RB/3922/2015/TAARIFA.
Mwanahabari wetu alipomtafuta meneja
huyo kuhusiana na tukio hilo, alikiri kuwa limemtokea lakini akasema
hakutaka kulivalia njuga lakini alichokifanya ni kutoa taarifa polisi
ili endapo atarudia, amchukulie hatua kali zaidi za kisheria.
“Ni kweli TID alinishambulia kwa
kunipiga kibao, iliniuma sana lakini nimeamua kumsamehe, nilichokifanya
ni kutoa taarifa polisi ili kama atarudia nimfikishe katika vyombo
husika,” alisema meneja huyo.
Jitihada za kumpata TID ili aweze kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.Jitihanada za kumpata Wambura hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa siku ya juzi.
Jitihada za kumpata TID ili aweze kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani.Jitihanada za kumpata Wambura hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa siku ya juzi.
tiko
tiko
Post a Comment