tiko
tiko
Pamoja
na mpango wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuliaga Bunge
kukwama jana, Chama cha ACT- Tanzania kimetangaza kukamilisha maandalizi
ya kumpokea mwanasiasa huyo kuanzia leo.
Mbunge
huyo alipanga kuliaga bunge na alisema amekwishapata ruksa ya Spika
kuwa angesimama bungeni kuwaaga wabunge na wanachama wa Chadema baada ya
chama hicho kumtimua uanachama wake hivi karibuni, lakini ghafla mpango
huo uliyeyuka kwa kile kilichoelezwa kuwa Spika amemkatalia.
Tangu
kuanzishwa kwa chama hicho mwaka mmoja uliopita, Zitto amekuwa
akihusishwa kukianzisha, hivyo kitendo chake cha kujiunga nacho
kitahitimisha mjadala wa muda mrefu wa mashabiki wake waliokuwa wakihoji
wapi ataelekea baada ya kung’olewa Chadema.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa ACT, Samsom Mgamba aliangua kicheko
na bila kuuma maneno alisema: “Hahahaa... tutampokea kuanzia kesho
(leo) na maandalizi yamekamilika.”
Alipotakiwa
kueleza wapi mapokezi hayo yatafanyika alisema: “Hilo mbona liko wazi,
yatafanyikia makoa makuu yetu (yapo Makumbusho, Dar es Salaam) lakini
kwa taarifa zaidi tutawajuza.”
Zitto
anaingia ACT ikiwa ni siku tisa kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi
wake mkuu, huku akitajwa kuwa ameandaliwa kushika wadhifa wa mwenyekiti
kuendeleza harakati zake za siasa.
Hivi
karibuni, chama hicho kilimvua uongozi aliyekuwa mwenyekiti
mwanzilishi, Lucas Limbu kutokana na mgogoro uliokuwapo baina ya
viongozi na kufanya nafasi hiyo kubaki wazi.
Tayari
washirika wa Zitto waliohusishwa naye kuandika waraka wa mapinduzi
ndani ya Chadema na baadaye kufukuzwa uanachama, Mwigamba na Profesa
Kitila Mkumbo wametua ndani ya chama hicho kipya.
Chama
hicho ambacho kinaendelea na uchaguzi katika ngazi ya mikoa kikibakiza
Mkoa wa Geita unaofanya uchaguzi wake kesho. Kitaanza vikao vyake vya
kitaifa Machi 27 na kuhitimisha kwa mkutano mkuu Machi 29.
Akizungumzia
uchaguzi huo, Mwigamba alisema: “Maandalizi yanakwenda vizuri na hakuna
shaka utafanikiwa kwa kiasi kikubwa na tunawaomba Watanzania watuunge
mkono.”
Tangu
juzi, Zitto alitarajiwa kuliaga Bunge lakini hakufanya hivyo kwa
kilichoelezwa kuwa aliitwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda na kupewa
ushauri kuwa afanye hivyo jana jioni.
Jana
asubuhi mbunge huyo hakuingika katika kikao cha Bunge lakini alionekana
katika viwanja vya Bunge akiwa amevaa shati la drafti na suruali ya
kaki akizungumza na rafiki yake wa karibu, Deo Filikunjombe ambaye ni
mbunge wa Ludewa kupitia CCM.
Katika
kipindi cha jioni, mbunge huyo aliingia katika viwanja vya Bunge saa
11:10 jioni akiwa amebeba mafaili huku akizungumza na simu na baadaye
kutaniana na waandishi wa habari waliokuwa nje ya ukumbi wa Bunge.
Mbunge
huyo aliyekuwa amevalia shati nyeupe na suruali nyeupe kabla ya kuingia
ndani ya ukumbi wa Bunge alizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya.
Akwama kuliaga Bunge
Habari
zilizopatikana bungeni jana jioni zilieleza kuwa Spika Bunge, Makinda
alimpiga ‘stop’ mbunge huyo kuaga bungeni bila kuweka wazi sababu za
kufanya hivyo.
Mbunge
huyo juzi alitinga bungeni kwa mara ya kwanza tangu Chadema kitangaze
kumvua uanachama na kufanya kikao cha siri na Makinda kwa zaidi ya saa
moja na baadaye kulieleza gazeti hili kuwa angezungumzia hatima ya
ubunge wake jana.
Habari
zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na watu wake wa karibu naye
zilieleza kuwa licha ya Makinda kumshauri mbunge huyo kuaga bungeni,
jana aligoma kumpa ruhusa hiyo.
“Kazuiwa
kuaga sijui kwa nini, ila kwa jinsi tunavyoona Makinda ni kama
anahitaji Zitto aendelee kubaki bungeni. Ngoja tusubiri kwanza tuone
nini kitatokea,” zilieleza habari hizo.
Alipoulizwa
juu ya taarifa hizo Zitto, alisema: “Hata mimi nasikia hivyo ila sina
hakika sana. Ngoja niende ndani nitajua zaidi, mimi nataka kuaga, can’t
stay any more (siwezi kuendelea kubaki).
Alipoingia
katika ukumbi wa Bunge, Zitto alionekana akizungumza na baadhi ya
wabunge wa upinzani na baadaye wakati mjadala wa muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji ukiendelea, alitoka nje na watu wa
karibu wa mbunge huyo walisema alikuwa akishinikiza kuaga kama
alivyopanga.
Spika
Makinda hakupatikana kuzungumzia sababu za kukataa kumruhusu mbunge
huyo na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alipoulizwa juu ya
suala hilo alisema hajui chochote.
Mbunge
wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage alisema mbunge huyo kisheria
hana mamlaka ya kushinikiza kuaga bungeni na kumtaka asubiri mamlaka
husika zifanye kazi hiyo, akimaanisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kulijulisha Bunge kuwa Zitto si mbunge tena baada ya kupata barua ya
Chadema.
Chadema
ilitangaza kumvua Zitto uanachama siku 10 zilizopita, saa chache baada
ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kutupa shauri lake alilofungua
akitaka chombo hicho cha sheria kimlazimishe katibu mkuu wa chama hicho
kumpa nyaraka za vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua nyadhifa zote.
Awali,
Mahakama hiyo ilitoa amri ya muda ya kuzuia Chadema kumjadili na
amedumu kwenye nafasi ya ubunge chini ya zuio hilo kwa takribani mwaka
mmoja.
tiko
tiko
Post a Comment