tiko
tiko
Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge mkoani Kagera, Seveline Niwemugizi amesema, viongozi wa dini wana haki ya kuwaelimisha waumini wao waweze kujua kinachoendelea wanapoona kuna mambo hayaendi sawa katika jamii.
Niwemugizi alisema pia wanayo haki ya kuwaambia waumini wao kuipigia
kura ya Hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ni wajibu wao kufanya
hivyo.
Akizungumza na gazeti la Mtazania, askofu Niwemugizi, alisema wao
kama viongozi wa jamii hawawezi kuona waumini wao wanapotea halafu
wanakaa kimya. Kufanya hivyo kutasababisha waingie kwenye uovu, alisema.
Askofu Niwemugizi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri wa Katiba
na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kuwataka maaskofu wasiwafundishe wananchi
jinsi ya kupiga kura bali wawaache watumie haki yao ya katiba kupiga
kura kulingana na utashi wao wenyewe.
“Sisi ni viongozi wa dini hatuwezi kuwaona kondoo wa Bwana wanapotea
halafu tukakaa kimya au kuwaacha, tutakuwa hatujatenda haki, lazima
tuwaambie waweze kuondoka kwenye kundi hilo na waweze
kujitambua,”alisema askofu huyo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza
la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).
Alisema hata viongozi wa serikali wanawaambia wananchi waipigie kura ya
NDIYO, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inalinda masilahi yao na kuhoji
haki hiyo ya kuwaelekeza hivyo wananchi wameipata wapi?
“Nimeshangaa kusikia kuwa Waziri anasema viongozi wa dini hatuna haki ya
kuwaambia waumini kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, mbona
Serikali imewaambia wananchi waipigie kura ya ndiyo, haki hiyo wameitoa
wapi,” alihoji.
tiko
tiko
Post a Comment