tiko
tiko
WATU
saba wanaodaiwa kuunda mtandao wa kigaidi Songea mkoani Ruvuma
wameshakamatwa na muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani kujibu mashtaka yanayowabili.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela alisema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa
wanadaiwa kuhusika na matukio matatu tofauti ya urushwaji na utegaji wa
mabomu ya kienyeji.
Alifafanuwa
kuwa tukio la kwanza lilitokea Septemba 16 mwaka jana majira ya saa
1.30 jioni huko katika eneo la Misufini kikundi hicho kinachojihusisha
na ugaidi kiliwarushia Askari polisi waliokuwa doria bomu la kienyeji la
kurushwa ambalo liliwasababishia askari watatu kujeruhiwa.
Alisema
kuwa katika tukio lingine ambalo lilitokea Oktoba 27 mwaka jana majira
ya saa 10 jioni lilichimbiwa ardhini bomu katika eneo la Mshangano
ambalo hutumiwa kama kituo cha ukaguzi wa magari
yanayotoka na kuingia Songea mjini na askari wa kikosi cha usalama
barabarani kando kando mwa Barabara inayotoka Songea kwenda Njombe kwa
lengo la kuwalipua askari wa kikosi hicho.
Kamanda
Msikhela alieleza zaidi kuwa pia kabla hawajatimiza hazma hiyo askari
wa usalama barabarani waliokuwa kwenye eneo hilo waliligunduwa bomu hilo
likiwa limechimbiwa ardhini na jeshi la polisi kwa kushilikiana na
jeshi la wananchi (JWTZ) baada ya kupata taarifa hiyo walifika kwenye
eneo la tukio na waliweza kuliteguwa bila kuleta madhara.
Alilitaja
tukio lingine la tatu kuwa lilitokea Disemba 25 mwaka jana majira ya
1.30 usiku katika eneo la Majengo Kotazi kikundi hicho cha ugaidi pia
kilidhamilia kuwarushia bomu askari waliokuwa wanafanya doria ambapo mtu
mmoja kutoka katika kikundi hicho alijaribu kuwarushia bomu askari hao
na kabla hajarirusha lilimlipukia yeye mwenyewe na kufariki Dunia papo
hapo na kusababisha askari polisa wawili kujeruhiwa vibaya.
Alieleza
zaidi kuwa timu ya upelelezi toka ndani ya jeshi la Polisi
kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimeweza kubaini
eneo linalotumika kwa mafunzo ya kigaidi na kikundi hicho na kwamba
mpaka sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo na wanatarajia kupanda
mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment