tiko
tiko
NI shida! Wakazi wa Mlandizi mkoani
Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita walijikuta wakishinda nje ya nyumba
moja ya kulala wageni iitwayo Kilimahewa Guest House baada ya kuwepo
taarifa za watu wawili, mtu na mpenzi wake kunatana baada ya kudaiwa
kufanya mapenzi majira ya asubuhi.
Mwananchi akitumia tochi kuwasaka uvunguni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
taarifa za kuwepo kwa tukio hilo zilisambaa kwa kasi na chanzo chake
kinadaiwa ni mwendesha pikipiki mmoja aliyetoa habari hizo.
Kutokana na uvumi huo, mamia ya watu
walijazana nje ya nyumba hiyo, huku wakisisitiza kutaka kuwaona watu
hao.“Saa 3 asubuhi kuna mtu mmoja wa pikipiki alikuja akatuambia kuwa
watu wamenasiana katika Gesti ya Kilimahewa, huwezi amini watu wametoka
Chalinze kwa ajili ya tukio hili na sisi harakaharaka tukafika hapa
kuona nini kinaendelea, mpaka sasa hatujui kama ni kweli ama sio kweli.V
“Polisi wamefika hapa wamesema hakuna
ukweli baada ya kuikagua gesti nzima lakini hata hatuamini tupotupo tu,”
walisema baadhi ya akina mama waliokuwa nje ya gesti hiyo, waliodai
wametokea Chalinze.
Diwani wa Kata ya Janga (CCM), Mlandizi,
Fedilia Swai alifika eneo la tukio baada ya kupokea taarifa na kukagua
kila chumba na aliwaambia wananchi kuwa hakuona chochote ndani ya gesti
hiyo na kwamba huo ni uvumi ambao hauna ukweli wowote na kuwataka watu
warudi makwao.
Muonekano wa kitanda walichokuwa wakitumia wapenzi hao.
“Unajua muda huu nilikuwa katika
shughuli nyingine, lakini ilinibidi nifike hapa baada ya kupata taarifa
kuwa kuna wananchi wangu wamenasiana. Nimeingia vyumba vyote hakuna kitu
kama hicho nimeingia na mashahidi wawili, mwanaume mmoja na mwanamke
mmoja tumekagua kote hakuna watu hao.
Nasisitika hizi taarifa ni za uongo tena uzushi mkubwa.”
Nasisitika hizi taarifa ni za uongo tena uzushi mkubwa.”
Kauli ya diwani huyo haikutosha mpaka
pale alipokuja tena mwenyekiti wa eneo hilo kwa tiketi ya Chama cha
Wananchi (CUF), Kilindo Ahmed ambaye pia alitoa kauli kama hiyo na
kuwataka wananchi hao kuteua wawakilishi wawili kwa ajili ya kwenda
kuthibitisha ndani ya nyumba hiyo.
Pamoja na mashahidi hao kueleza ukweli wa kutokuwepo kwa tukio hilo, bado wananchi hawakuamini.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdallah Saidi alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma ili akose wateja katika biashara yake.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdallah Saidi alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma ili akose wateja katika biashara yake.
...Wananchi wakisubiria kwa nje.
“Kuna watu wamesambaza uvumi huu
makusudi ili kuniharibia biashara yangu, huu ni mpango wa kunichafua
kibiashara, angalia siku nzima sijafanya kazi yoyote, wateja wangu
wataanza kuogopa kuja,” alilalama mmiliki huyo.
tiko
tiko
Post a Comment