tiko
tiko
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeshusha kidogo bei ya umeme kuanzia Machi Mosi mwaka huu, huku ikisisitiza kwamba bei hiyo itaendelea kupungua zaidi mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam utakapoanza kazi.
Taarifa
za hivi karibuni, zimeeleza kuwa bomba hilo limekamilika kwa asilimia
99 na kinachosubiriwa ni pamoja na majaribio ya usafirishaji wa gesi
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Ewura, Felix Ngamlagosi, alisema kushuka kwa gharama hizo kunatokana na
mabadiliko ya gharama za Shirika la Umeme (Tanesco), kutokana na
mabadiliko katika bei ya mafuta, thamani ya fedha na mfumuko wa bei.
“Ukilinganisha
makadirio yaliyofanywa na Ewura mwaka 2013, mahitaji ya pato la Tanesco
kwa mwaka 2014 yanapunguzwa kwa kiasi cha Sh bilioni 33. Punguzo hili
linashusha bei ya umeme ya wastani kutoka Sh 257.39 kwa uniti moja hadi
Sh 251.70 kwa uniti moja sawa na asilimia 2.21,” alisema.
Alisema
kwa wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya umeme itashuka kutoka Sh
306 kwa uniti hadi Sh 298 kwa uniti sawa na punguzo la Sh nane.
Kwa
bei hiyo ya watumiaji wa kawaida, umeme wa Sh 10,000 kwa bei ya zamani
mtumiaji alikuwa akipata uniti 32.67, sasa kwa bei hiyo atapata uniti
33.5, ambayo ni ongezeko la uniti 0.88.
“Kwa
wateja wenye matumizi ya kawaida kwa kupitia volti 400, bei ya umeme
itashuka kutoka Sh 205 kwa uniti hadi Sh 200 kwa uniti sawa na punguzo
la Sh tano kwa uniti,” alisema.
Alisema
kwa wateja waliounganishwa katika msongo wa kati wa umeme, bei ya umeme
itashuka kutoka Sh 163 kwa uniti hadi Sh 159 kwa uniti sawa na punguzo
la Sh nne kwa uniti moja.
Ngamlagosi
alisema kwa wateja waliounganishwa katika msongo mkubwa wa umeme,
vikiwemo viwanda, migodi na Zanzibar bei ya umeme itashuka kutoka Sh 159
kwa uniti hadi Sh 156 kwa uniti sawa na punguzo la Sh tatu kwa uniti.
“Kwa
wateja wa majumbani wenye matumizi madogo ya wastani wa uniti 75 kwa
mwezi, bei ya umeme haitabadilika kutokana na kwamba kundi hilo bei yake
ni chini kutokana na gharama zake kuchangiwa na kundi la wateja wakubwa
wa majumbani,” alisema.
Ngamlagosi
alisema Desemba 10 mwaka 2013 Bodi ya Wakurugenzi ya Ewura ilitoa agizo
la mabadiliko ya bei ya umeme unaouzwa na Tanesco kwa kipindi cha miaka
mitatu kuanzia 2014 hadi 2016 na zilianza kutumika mwaka jana.
Alisema
kulingana na agizo hilo na kipengele cha saba cha kanuni za Kupanga Bei
ya Umeme, bei za umeme zinatakiwa kurekebishwa kila baada ya miezi
mitatu, kutokana na mabadiliko ya bei ya mafuta, thamani ya Shilingi ya
Tanzania na mfumko wa bei na marekebisho hayo yanahusu bei ya kununua
uniti ya umeme na si kwa tozo za mwezi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment