tiko
tiko
SERIKALI imesema inaendeleza jitihada za kuachana na matumizi ya nguzo za umeme za miti, badala yake itatumia nguzo za zege ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha huduma ya usambazaji na upatikanaji wa umeme nchini.
Hayo
yalibainika mwishoni mwa wiki katika kikao baina ya uongozi wa Kampuni
ya Sunshine Group Ltd na wataalamu wa sekta ya umeme kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
Katika
kikao hicho, Kampuni ya Sunshine iliwasilisha mapendekezo ya kuanzisha
kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya
nchini.
Akieleza
msimamo wa Serikali kuhusu mapendekezo hayo, Kamishna Msaidizi wa
Umeme, Innocent Luoga alisema Serikali ina dhamira ya kutumia nguzo za
umeme zilizotengenezwa kwa zege na kuachana na za miti zinazotumika sasa
kutokana na manufaa yake.
Luoga aliyataja manufaa ya kutumia nguzo za zege kuwa ni pamoja na uimara wa nguzo husika.
“Huwezi kulinganisha uimara wa nguzo za zege na hizi za miti tunazotumia hivi sasa. Nguzo za zege ni madhubuti na imara zaidi,”alisema.
Akifafanua, Luoga alisema kutokana na uimara wa nguzo za zege, uhai wake ni wa muda mrefu kulinganisha na nguzo za miti.
“Uhai wa nguzo za zege ni kati ya miaka 70 hadi 100, wakati uhai wa nguzo za miti ni miaka 50,” alisema
Luoga na kusisitiza kuwa sifa hiyo ya uhai mrefu wa nguzo za zege
inazalisha manufaa mengine kwa Serikali na wananchi kwa ujumla endapo
nguzo hizo zitatumika.
Faida
nyingine za kutumia nguzo za zege, zilizotajwa na wataalamu katika
kikao hicho ni pamoja na kuwa rafiki wa mazingira ambapo huepusha
ukataji wa miti.
Nyingine
ni uwezo wake wa kutopitisha maji na kutoshika moto kwa urahisi.
Akihitimisha mazungumzo husika, Luoga alisema Serikali itaendelea
kufanya mazungumzo na kampuni hiyo na wawekezaji wengine wenye nia ya
kutengeneza nguzo za umeme za zege ili kufikia makubaliano
yatakayowezesha pande zote mbili kunufaika.
“Mkakati
wetu ni kwa Tanesco kutengeneza nguzo za zege kwa matumizi ya ndani ya
nchi lakini ni vyema tukapata wawekezaji wengine watakaosaidia
kutengeneza nguzo hizo kwani mahitaji ni makubwa sana,” alisema.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment