tiko
tiko
Inadaiwa kuwa kimenuka kati ya msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ na baba mwenye nyumba wake, Hussein Kassim baada ya mdada huyo kudaiwa kugoma kutoa vyombo vyake kwenye mgahawa aliopangishwa na mkataba kuisha.
Ray
C aliyekuwa akitoa huduma ya chakula na vinywaji kwa wafanyakazi wa
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kupitia mgahawa wake maarufu kwa
jina la Ray C Restaurant, alifikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa na
yeye alipwe fidia ya shilingi laki moja kwa ajili ya ukarabati
alioufanya.
Akizungumza na Ijumaa,
baba mwenye nyumba hiyo alisema baada ya Ray C kugoma kutoa vitu vyake,
aliamua kwenda kumshtaki kwa mabosi wao wa kitengo cha Methadone
ambacho kinamtibu Ray C na yeye mwenyewe kwani wote ni waathirika wa
madawa ya kulevya.
Baba
mwenye nyumba huyo alidai baada ya kumshtaki katika kitengo hicho, Ray C
aliahidi kwenda kuvunja ukuta ambao aliujenga na kuchukua vitu vyake
hivyo baada ya siku mbili na angepeleka ufunguo kwa mkuu wa kitengo cha
Methadone.
“Mkataba
uliisha Januari 19, mwaka huu lakini akakaa kimya mpaka nilivyoenda
kumwambia maana alikuwa ameshikilia ufunguo wangu huku mimi nimeshapata
mteja mwingine.
“Kila
nikimwambia aje kutoa vitu vyake anakataa na kusema mpaka nimlipe laki
moja aliyofanyia ukarabati wakati mimi hakunishirikisha, sikutaka kufika
huku maana Ray C ni mwenzangu tunakunywa naye dawa lakini ukorofi wake
ndiyo umesababisha haya yote,” alisema Hussein.
Baada
ya siku mbili kupita, mkuu wao alimtaka aende kisheria ambapo alienda
kuripoti katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Minazini, Mwananyamala na
Ray C akaandikiwa barua ya wito mara ya kwanza, hakwenda baada ya hapo
akaandikiwa kwa mara ya pili, Jumanne iliyopita ambayo alifika akiwa
amechelewa.
Ray
C baada ya kuambiwa dhumuni la wito huo kwa afisa mtendaji, aliahidi
kutoa vitu hivyo siku iliyofuata.Alipoulizwa Ray C kuhusiana na tukio
hilo, alikiri kupelekwa serikali ya mtaa na kusema vitu vingi
vinavyoongelewa dhidi yake havina ukweli.
“Hayo
wanayozungumza ni mambo ya Kiswahili tu, mimi nimeshaachia fremu ila
bado kuchukua vitu vyangu tu, nenda serikali ya mtaa utapata maelezo
kamili maana hao wanataka kunichafulia jina tu,” alisema Ray C.
Credit:Gpl/Ijumaa
Credit:Gpl/Ijumaa
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment