tiko
tiko
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi,
Mkoa wa Mwanza, Mansoor Mohamed (25) amefikishwa Mahakama ya Wilaya kwa
tuhuma za shambulio la kudhuru mwili.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Eliasha Kisura alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa
hilo Februari 10 saa 7:00 mchana kwa kumshambulia kwa mateke na ngumi
Katibu wa UVCCM Wilaya, Nassoro Mohamed kinyume cha sheria.
Baada
ya kusomewa mashtaka, mshtakiwa alikanusha na Hakimu Mfawidhi, Godfrey
Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 25 itakapoanza kusikilizwa.
Mshtakiwa
aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini
wawili wenye mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh700,000.
Chanzo cha ugomvi
Chanzo
cha ugomvi inadaiwa ni kambi za ubunge ndani ya UVCCM wilayani humo,
hali inayoonyesha Mwenyekiti wa umoja huo, Mansoor Mohamed kutofautina
na Katibu wake, Mohamed Nassoro.
Mohamed inadaiwa alishtukia kikao cha makatibu wa vijana ambacho kiliitishwa na Nassoro bila kumtaarifu yeye kama mwenyekiti.
Inadaiwa
Mohamed alivamia kikao hicho cha makatibu wa kata wilayani hapa,
kilichokuwa kinafanyika Ukumbi wa CCM na baada ya kumhoji katibu wake
sababu za kuitisha kikao bila kumpa taarifa, walianza kurushiana maneno
makali na kuanza kupigana.
Akizungumza
kwa simu jana baada ya tukio hilo, Mohamed alisema alipata taarifa za
kikao hicho kutoka kwa wajumbe, hivyo akalazimika kwenda ukumbini kujua
sababu za katibu wake kushindwa kumpa taarifa.
“Nimepokea
ujumbe wa simu kutoka kwa makatibu wa UVCCM kuwa kuna kikao, mimi sina
taarifa yoyote nilikwenda kufahamu sababu za kunificha taarifa hizo,”
alisema Mohamed.
Mohamed
alisema kinachoendelea ni suala la makambi ya wagombe ubunge kuelekea
uchaguzi mkuu Oktoba, kwani akiwa kiongozi wa UVCCM hawezi kukubali
kuona kanuni na taratibu zikikiukwa wilayani kwake akanyamaza.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment