tiko
tiko
Thank you God! Neno
pekee unaloweza kusema ni Mungu mkubwa baada ya kusikia taarifa kwamba
mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake
imetengemaa, Ijumaa Wikienda lina kitu kamili.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo,
kililieleza gazeti hili kwamba, tayari Sandra amesharejea katika hali
yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa
hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.
Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini
wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari
kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali
aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na
familia yake.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
Mama na mwana wakiwa ni wenye furaha baada ya kukutana tena.
“Mama amerejea juzikati kutoka kwenye matibabu nchini India alikokuwa
amepelekwa, hivyo tunamshukuru Mungu sasa anaendelea vizuri na afya yake
kwa jumla inaridhisha ingawa ana programu ya kufanya mazoezi mepesi ili
aweze kuimarika zaidi ya vile alivyokuwa awali.
“Pia kuna dawa ambazo alipewa kwa ajili ya kumpatia nguvu zaidi,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa ombi la kutotajwa gazetini.
“Pia kuna dawa ambazo alipewa kwa ajili ya kumpatia nguvu zaidi,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa ombi la kutotajwa gazetini.
Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa mama Diamond ambapo
lilihakikishiwa kwamba bimkubwa huyo alikuwa ndani amelala na Diamond
yupo nchini Afrika Kusini kikazi
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment