tiko
tiko
kitaka kujua hali yangu, mimi sijambo.
Mzima wa afya na ninaendelea na majukumu yangu ya kila siku.
Nimekukumbuka leo kupitia barua, maana kitambo kidogo hatujakutana ana
kwa ana kikazi.
Nimekukumbuka Madam sababu natambua
uwepo wa shindano lako kubwa la Bongo Star Search. Msisimko wake ni
mkubwa na ndiyo maana Watanzania huwa wanalifuatilia kwa ukaribu pale
linaporindima nchi nzima.
Big up kwa mchango wako maana mbali ya
mshindi kupatikana na kupata chapaa, huwa kunakuwa na burudani nzuri
hususan kutoka kwa washiriki ambao hugeuka kuwa ‘komedi’ kutokana na
vituko vyao.
Pamoja na kukupa pongezi hizo lakini pia
nina jambo nataka kukukumbusha. Kwa kuwa mwaka jana shindano hilo
halikufanyika kwa kile ulichokiita kuwa ni ucheleweshwaji wa taarifa za
wadhamini kutoshiriki, umeeleweka lakini swali ni kwamba., mwaka huu je
umejipangaje? Jibu najua unalo.
Wakati ukitafakari juu ya ujio wako
mpya, ni vyema pia ukatafakari pia juu ya ufanisi kwa kujifunza kupitia
mashindano ya miaka iliyopita. Changamoto zote, malalamiko yote
uyafanyie kazi. Watu wanataka kuona burudani na mshindi anapatikana
kihalali.
Wanataka kuona kweli yule mshindi ambaye
ana sifa za kuwa mshindi ndiye anayevishwa taji. Najua pengine kutokana
na majukumu yako, yawezekana usiwe unayasikia malalamiko yote
yanayoibuliwa na wananchi huku mitaani ila usijali nitakufikishia maana
mimi ni balozi wao.
Kelele za watu wengi huwa ni mshindi
kuwa tofauti na yule ambaye wengi wanaamini ana uwezo. Jitahidi sana
hilo lisitokee mwaka huu. Jitahidi kusimamia majaji wasipendelee.
Wampate mshindi ambaye kweli ana vigezo vya kuimba na asije hata
kukuangusha, awike kimuziki na si kupotea mara tu shindano
linapomalizika.
Kama unaona kuna udhaifu katika majaji
ni vyema ukawashirikisha wataalam kutoka Balaza la Sanaa Nchini (Basata)
ili waweze kutoa mawazo yao kitaalam.
Kiwango cha zawadi pia huwa ni tatizo.
Kumekuwa na uvumi wa muda mrefu kwamba zawadi inayotangazwa si ile
anayokabidhiwa mshindi, hivyo ni vyema basi mwaka huu uzushi huo
ukatafuta namna ya kuufanya ufikie mwisho.
Ni bora kutangaza zawadi ndogo lakini
ikamfikia yote mshindi kuliko kutangaza kubwa halafu kiuhalisia anapewa
ndogo. Mfumo wa kupiga kura uwe wazi na kila mtu aamini kabisa kwamba
ushiriki wake katika kupiga kura una maana. Kusiwe na chembe ya
ujanjaujanja.
Kwa leo naishia hapa.
Kwa leo naishia hapa.
tiko
tiko
Post a Comment