tiko
tiko
BWENI la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi iliyoko Jimbo la Isimani Wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa, limeteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi, ikiwa ni miaka sita tu tangu bweni hilo liungue na kusababisha hasara kubwa na vifo vya wanafunzi 13.
Agosti
25, 2009 bweni la shule hiyo, liliwaka moto na kusababisha vifo vya
wanafunzi wa kike 13, ambao baadhi yao walizikwa shuleni hapo baada ya
miili yao kuharibika vibaya.
Katika
tukio hilo, wanafunzi wengine 23 walijeruhiwa vibaya, baada ya bweni
hilo kushika moto uliosababishwa na mshumaa uliowashwa na aliyekuwa
mwanafunzi wa shule hiyo, Naomi Mnyali ambaye alisahau kuuzima baada ya
kumaliza kusoma.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto
mkoani Iringa, Inspekta Kennedy Komba alisema kuwa bweni hilo
limeteketea lote na kuunguza baadhi ya mali, zikiwemo za wanafunzi
zilizokuwemo katika bweni hilo.
Alisema
taarifa za awali zinaonesha chanzo cha moto huo, kilitokana na hitilafu
ya umeme na kwamba hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa katika tukio
hilo.
Komba
alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa ya tukio hilo,
lililotokea kati ya saa 3 na 4 jana asubuhi wakati wanafunzi wa shule
hiyo wakiwa darasani, iliwachukua dakika 45 kufika katika eneo la tukio.
Alisema
baada ya kufika katika eneo la tukio kutoka Iringa mjini ambako ni
umbali wa kilometa 40, kazi ya kuuzima moto huo haikuwa kubwa, kwani
wananchi waliofika kutoa msaada, walifanikiwa kuzima moto huo kwa kiasi
kikubwa.
Aliwapongeza
wananchi kwa moyo wa ushujaa wa kujitolea na kuwataka kutoa taarifa
mapema pindi majanga ya moto, yanapojitokeza katika maeneo
yanayowazunguka.
“Endapo tungepata taarifa mapema ninaamini tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi,” alisema
Kamanda huyo na kuwataka wananchi wasitegemee mtendaji au kiongozi
apige simu kwa kikosi cha kuzima moto kwani kila mtu ana fursa ya kupiga
simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha jeshi hilo kuweza kutoa
taarifa ya majanga.
Aliongeza
kuwa walitumia muda mdogo kufika eneo la tukio, kutokana na ubora wa
gari walilokuwa nalo na kuwashukuru wananchi kwa taarifa na kuweza
kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo usilete madhara zaidi.
Akizungumzia
hasara iliyosababishwa na moto huo, Komba alisema tathmini kamili ya
mali zilizoteketea, itafanywa kwa kushirikiana na uongozi wa shule na
taarifa yake kutangazwa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment