tiko
tiko
Kutokana na
upungufu wa madarasa ya kusomea wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha
pili katika shule ya sekondari matarawe iliyoko Songea mkoani Ruvuma
wanasomea kwenye maabara zilizojengwa kwa agizo la Rais Kikwete na
wanalalamikia hatua hiyo kutokana na kuumia kwenye mifereji ya maabara
hizo.
Uchunguzi wetu
umebaini hilo na wanafunzi wamesema kuwa wamekuwa wakisoma kwa shida
kwa kuwa vyumba hivyo si rasmi kwa kusomea hivyo wameomba kujengewa
madarasa.
Diwawani wa kata
ya matarawe Bw.James Makene amesema kuwa wameamua kugeuza maabara kuwa
madarasa kwa kuwa hawana madarasa ya kutosha ilhali mwaka huu wamepokea
wanafunzi mia mbili wa kidato cha kwanza.
Hata hivyo
vyumba hivyo vya maabara awali vilikuwa madarasa na vimekarabatiwa ili
viwe maabara huku ukarabati wake ukilalalamikiwa kwa madai kuwa uko
chini ya kiwango.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment