tiko
tiko
NIJumanne tena! Kweli siku hazigandi kwani mara nimalizapo kuandika safu
hii, kufumba na kufumbua siku ya kuandika tena inafika!Baada ya wiki
iliyopita kumalizana na mada ya Mke Kumchuna Mume Ipo Sana! Leo nashuka
na mada nyingine. Hii ni kwa wapenzi, wachumba au wanandoa.
Kila
mtu anajua maisha ya sasa kuhusu mawasiliano ni simu za mikononi. Simu
hizi zimekuwa mwiba katika baadhi ya uhusiano kutokana na baadhi yao
kuzitumia kwa usaliti lakini kwa wengine maisha yanaendelea.
Nilikaa nikatafakari malalamiko niliyowahi kuyasikia siku za nyuma na
hata karibuni, kwamba baadhi ya wapenzi wameingia kwenye mgogoro kuhusu
simu kufuatia kupigiwa na wenza wao halafu hawapatikani hewani au
hawapokei tu!
MSINGI WA MANENO NI USALITI
Tabia hii, kila mwenye simu amewahi kukumbana nayo na pengine imewahi kuvunja ndoa kabisa. Wengi wanaamini wenza wao kutopokea simu kunatokana na kuwepo pengine gesti au sehemu nyingine tete kwa hiyo simu ameweka mbali kwa sababu anabanjuka.

Wengine wanaamini ni dharau! Kwamba, mwenza wake anaiona simu ikiita
lakini hataki tu kupokea kwa sababu zake binafsi! Hii pia imekuwa
ikisababisha ugomvi kwa wapendanao.
UKWELI NI UPI?
Nilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wasomaji wangu kuhusu hili ambapo baadhi walisema ni afadhali simu ya mwenza wake iite kwa muda mrefu bila kupokelewa kuliko isiwe hewani!
Nilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wasomaji wangu kuhusu hili ambapo baadhi walisema ni afadhali simu ya mwenza wake iite kwa muda mrefu bila kupokelewa kuliko isiwe hewani!
“Mimi
binafsi kwangu, nikimpigia mume wangu afadhali simu yake iite tu hata
mara kumi lakini nisimkose hewani. Ninapomkosa hewani mume wangu nahisi
yuko gesti na mwanamke mwingine,” alisema mama Lizi, mkazi wa
Makumbusho, Dar.
“Mimi tofauti na huyo. Mimi pia afadhali simu iite asipokee kuliko
kutokuwa hewani, ila sasa asipokuwa hewani siwazi yuko gesti, bali
nawaza amekumbwa na janga zito, pengine hata kifo,” anasema baba Frank,
naye mkazi wa Makumbusho.
Mama Mudy, anaishi Kimara-Korogwe, Dar. Yeye anasema: “Mimi mume wangu
akitaka tugombane simu yake iite asipokee. Afadhali nipige nigundue
haipo hewani kwani anaweza kunidanganya ilizima yenyewe maana si unajua
simu zetu za Kichina hizi.”
“Kusema kweli mimi nikimpigia simu mke wangu halafu ikawa haipatikani
hewani nakuwa na amani kuliko asipokee. Maana najua anaiangalia tu na
anajua anayepiga ni mimi, nakuwa naumia sana,” anasema Ibrahimu, mkazi
wa Buguruni-Kisiwani, Dar.
TABIA INACHANGIA
Nilichobaini ni kwamba, ugomvi wa kutopokea simu wakati inapatikana hewani unatokana na tabia ya mmiliki wa simu. Baadhi ya watu wanajulikana kuwa, hakai mbali na simu yake hata kwa dakika mbili, sasa ikitokea mwenza wake anapiga hapokei anajua anafanya makusudi kwa vile inaaminika hawezi kuwa mbali na simu kwa muda mrefu.

Mama Salama, mkazi wa Sinza D, Dar yeye alisema: “Niliwahi kugombana na
mume wangu, eti nilimpigia simu ikaiita wee mpaka nikaacha. Halafu
ikapita nusu saa hajapiga wakati najua si kawaida yake kuwa mbali na
simu.”
Itaendelea wiki ijayo, usikose.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment