tiko
tiko
Kichwa! Staa
bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta
jijini Dar.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo,
mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina
lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema
kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa
chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,”
alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama
supastaa.
tiko
tiko
Post a Comment