tiko
tiko
SELFIE
ni kama ndio neno la mjini hivi, watu na simu zao basi ni full
kujiachia, wanapiga selfie zao halafu wanashare Instagram na watu wao
basi inakua poa tu yani.
Unajua teknolojia inarahisisha maisha kila siku, sikuwahi kufikiria kwamba kuna siku hizi selfie zitachukua nafasi ya passport size!
Mara nyingi tunazitumia passport size
kwenye vitambulisho vyetu au cheti hivi au sehemu yoyote inapotakiwa,
nakusogezea hii kutoka Uingereza ambako Benki ya Lloyds imeanzisha
utaratibu huu, kama unataka kufungua account huna haja ya kupiga
passport size, selfie yako moja tu basi kazi imeisha.
Mteja atakachotakiwa kufanya ni kupiga
selfie yake moja na pia kupiga picha ya passport iliyo kwenye leseni, au
kitambulisho chochote halafu anatuma, kompyuta ikitambua tu kwamba
picha hizo mbili ni za mtu mmoja basi mteja anaendelea zake na taratibu
nyingine kufungua account mpaka inapokamilika.
Tunajua kwamba watu wako busy na
majukumu ya kimaisha duniani kote, Uingereza wameifurahia hii, wanasema
ni rahisi na itaokoa sana muda wao kukamilisha kila kitu mtandaoni
wakati wa kufungua account.
Natamani niione hii Bongo siku moja, hapo vipi mtu wangu?
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment