tiko
tiko

SIKU chache baada ya picha za mtoto mchanga kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa ni za mtoto wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kuwa amezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hatimaye wawili hao wamefunguka.
Hatua
hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika mgogoro wa
ndoa yao hali iliyosababisha mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kufikishwa
mahakamani kwa kosa la ubakaji.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana ili kupata ukweli kuhusu taarifa za picha za
mtoto huyo ambaye anadaiwa kuwa amezaa na Flora, Mchungaji Gwajima,
alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa
Flora.
Mchungaji
Gwajima alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo unaosambazwa
dhidi yake kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora anamwachia Mungu kila
kitu.
“Hahaha… si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu… wakati mwingine mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.
“Hahaha… si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu… wakati mwingine mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.
“Awali
niliwaza kuwashitaki (alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na
Flora) wanaoeneza uzushi huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’
(haina mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,”alisema Mchungaji Gwajima.
Alipoulizwa kuhusu mtu anayemshuku kueneza uvumi huo alisema:“Probably’
(nadhani) atakuwa Emmanuel Mbasha mwenyewe. Tangu mwanzo alipotuhumiwa
kumbaka shemeji yake na kutoroka kwake akihofia kukamatwa na polisi,
mkewe alikuja kanisani kwetu na mimi nilimwagiza mwenyekiti wa kusaidia
jamii amsaidie,” alisema Gwajima na kuongeza:
“Sasa Mbasha alipotoka huko alikokimbilia na kusikia kuwa mkewe yuko hapa kanisani, ndipo alipoanza kueneza uzushi,” alisema.
Gwajima alisisitiza kuwa Flora hakufikia kwake kwa jambo lolote bali aliendelea kuishi katika nyumba aliyopanga.
Alipoulizwa
kwa nini hamshitaki Mbasha ili kulinda heshima yake, Gwajima alisema
ameshawaita ndugu zake akiwemo baba yake mzazi lakini nao wakaonekana
kutommudu Emmanuel.
“Nilishawaita
wazazi wake, baba na mama yake, ndugu zake kina Mbasha na tukazungumza.
Lakini baba yake alisema hata yeye amemshindwa. Yaani anawadharau hata
ndugu zake,” alisema.
Akisimulia
jinsi alivyokutana na Emmanuel na Flora Mbasha, Mchungaji Gwajima
alisema awali walikuwa wakiimba kwenye mikutano aliyokuwa akihubiri.
“Hawa
hawakuwa washirika wetu, ila walikuwa wakija kuimba kwenye mikutano
yetu ya Injili. Walikuja Arusha, Moshi na Tanga, kwa hiyo tulikuwa
tukiwatumia sana. Baadaye ndiyo yakatokea hayo hadi Flora akakimbilia
kanisani kwetu,” alisema.
Hata hivyo Gwajima alisema hakujua kama Flora ni mjamzito wakati anakuja kuomba msaada kanisani kwake.
“Mimi
sikujua kama alikuwa mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndiyo
nazisikia kwako. Hapa nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam,” alisema na kuongeza:
“Sasa kama mtu una wasiwasi na mtoto si ukapime DNA ili upate uhakika? Hii ni habari ya kutaka tu kulichafua kanisa na huduma,”alisisitiza.
Flora anena
Mwandishi alimtafuta Flora kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hilo ambapo alisema “Siko
tayari kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa. Yeye anajeuri ya pesa
ndo maana anafanya haya yote lakini mimi ninasimama na Mungu wangu na
ninajua Mungu atanipigania,” alisema Flora.
Alipoulizwa kuhusu hali ya mtoto wake mchanga, alisema “Mtoto hajambo, lakini mtoto anayesambazwa kwenye mitandao siyo wangu, na hizo picha nyingine nafikiri ni za kutengeneza tu,” alisema Flora.
Mbasha
Kutokana
na hali hiyo Mwandishi alimtafuta mume wa Flora, Emmanuel Mbasha, ili
kuzungumzia suala hilo, licha ya kupokea simu yake ya kiganjani,
aliishia kusema yuko njiani hivyo apigiwe baadaye.
Hata alipopigiwa baadaye, aliendelea kusema kuwa atafutwe baadaye na wala hakujibu ujumbe wa simu (sms).
Alipotafutwa
kwa njia ya ujumbe mfupi wa WhatsApp, ujumbe huo ulionekana kufika na
kusomwa na baada ya muda alituma ujumbe wa sauti uliokuwa na wimbo na
kuandika maneno mafupi yaliyosomeka ‘wimbo wangu mpya’.
Pamoja na mambo mengine, wimbo huo unamaneno yasemajo “Haribu mipango ya shetani, haribu…, Binadamu wengine mashetani mfano wa Cobra, wanawaza mabaya, kuna siku watakufa kabisa,” ulisikika ujumbe wa wimbo huo
Sehemu nyingine ya wimbo huo ulioimbwa kwa mwelekeo wa mipasho, inasema “Wanakesha kwa waganga kuliloga, darubini ya bwana imewamulika, ukiwaona utadhani ni wema,”
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopo katika tovuti ya kituo cha televisheni ya
East Africa (EATV), Agosti 27, mwaka jana Flora alihojiwa na kituo hicho
kupitia kipindi cha Kikaangoni Live, kinachoendeshwa kwa njia ya
mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema ujauzito aliokuwa nao ni wa
mumewe Mbasha na si Mchungaji Gwajima.
Flora
alisema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji Gwajima
kwa kuwa ni mjomba wake na kwamba watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la
kumchafua na kumshushia hadhi.
“Hayo
ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji Gwajima ni mtumishi wa Mungu
na ni ‘Uncle’ wangu ninawezaje kuwa na uhusiano na uncle wangu..? ” alihoji Flora.
Kuhusu
kuachana na Mbasha, Flora alisema hakuachana naye kwa sababu ya Gwajima
na amedai kuwa bado anampenda, lakini anampenda Mungu zaidi.
“Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu,” alisema Flora.
tiko
tiko
Post a Comment