tiko
tiko
MSANII mkongwe
katika tasnia ya maigizo Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amefunguka
kuwa anasubiri kwa hamu usajili wa fomu ukamilike ili aweze kugombea
tena uongozi wa Klabu ya Bongo Movie.
Akipiga stori na Uwazi, Dk. Cheni
aliweka wazi kuwa ameanza kuona ndoto zake za kuiongoza klabu hiyo
zitatimia kwa asilimia fulani kama ambavyo alikuwa akitamani kuwa
kiongozi kwa muda mrefu.
“Niko tayari na nitagombea tena uongozi
kwa nafasi ya uenyekiti, sasa hivi ninachosubiri ni usajili tu
ukikamilika na mambo yatakwenda sawa kwani nimejipanga vya kutosha
kuongoza,” alisema Dk. Cheni.
tiko
tiko
Post a Comment