tiko
tiko
Kwanza nianze makala haya kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima leo. Ahimidiwe daima.
Baada ya kusema hayo niseme wazi kwamba nchi yetu ilitikisika tena wiki iliyopita baada ya polisi wetu kuwapiga Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake.
Baada ya kusema hayo niseme wazi kwamba nchi yetu ilitikisika tena wiki iliyopita baada ya polisi wetu kuwapiga Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake.
Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa
sheria na kanuni, haitakuwa busara kila mtu kujifanyia mambo yake
anayotaka bila kuzingatia sheria na hasa askari wetu.Ningefurahi kama
vyombo husika vitafanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na
ikibainika kuwa polisi walitumia nguvu kubwa wawajibishwe kwa mujibu wa
sheria.
Binafsi na wapenda amani wote katika
nchi hii bila kujali itikadi za kisiasa tunalaani vikali kitendo cha
kupiga raia kama mbwa mwitu.
Naamini yeyote aliyeona tukio lile kwa
njia ya video alisikitika, alishangaa na kuingia woga kwa sababu hakuna
aliyekuwa anategemea kuona askari wetu wakifanya vitendo ambavyo
vilikuwa vikifanywa na askari wa Makaburu dhidi ya Waafrika kule Afrika
Kusini.
Kwa nini askari umpige mtu ambaye ametii
sheria au amri ya kukamatwa bila shuruti wakati huo ndiyo msemo wa
jeshi la polisi?Kwa tukio hili ni lazima serikali isimamie sheria bila
kupendelea mtu yeyote. Nasema hivyo kwa sababu suala la amani ya nchi ni
suala la kitaifa na halitakiwi kuingizwa kwenye siasa, hivyo nawasihi
viongozi wa polisi kuwa makini na suala hilo ambalo limetia doa nchi
yetu.
Nasema limetia doa kwa sababu hata sasa
ukifungua mitandao mbalimbali duniani ikiwemo ya Voice of America (VoA),
polisi wetu wanaonekana wakiwapiga raia hata bila kujali wanapiga
sehemu gani. Tumshukuru Mungu, hawakuua!
Lakini yeyote aliyeona video ile ni
lazima atapata hasira kwa askari wale wachache waliokiuka sheria ya
ukamataji raia waliokosa.Nisisitize tu kwamba amani na usalama wa nchi
yetu ni kitu muhimu sana katika ustawi wa taifa letu, lakini kila siku
tunashuhudia kuendelea kuporomoka kwa amani na usalama, ninawasihi
wananchi wenzangu, tunapojadili suala kama hili lazima tuweke kando
itikadi zetu, lengo likiwa kuliponya taifa.
Nisisitize kuiomba serikali kufanya
uchunguzi kupitia vyombo vyake, pia bunge lichunguze sheria ambazo
zinatoa mwanya wa vurugu ili kudhibiti vitendo hivyo.Suala hili ni nyeti
kwa sababu limeweka bayana kugongana kwa mihimili mitatu ya nchi baada
ya Bunge kujadili suala hilo wakati likiwa limeshafika mahakamani.
IGP Mangu.
Mgongano huo umetokea katika kipindi
kisichozidi miezi miwili baada ya Bunge kugoma kupokea zuio la mahakama
la kujadili kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escow na
kuendelea na mjadala ambao ulifikia maazimio ya kuwawajibisha wahusika.
Sitamzungumzia Profesa Lipumba juu ya
kukamatwa kwake Jumanne iliyopita wakati akielekea Zakhem, Mbagala Dar
kwa sababu shauri lake lipo mahakamani.Licha ya shauri hilo kuwa
mahakamani, wabunge walijadili kwa kina tukio lote la kupigwa na
kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi
Tanzania lilifanya haraka kuwahisha shauri hilo mahakamani na kitendo
hicho wachunguzi wa habari wanasema kililenga kulizuia Bunge kutekeleza
azma yake ya kujadili tukio hilo.
Jeshi la polisi halipaswi kutumia nguvu
kuliko zinazohitajika katika kukamata watuhumiwa wa makosa ya jinai hilo
halipo kwenye sheria naambiwa ipo kwenye maagizo ya jumla ya polisi
yaani Police General Orders.
Ukweli ambao upo wazi ni kwamba sheria haiwapi polisi mamlaka ya kupiga raia anayetii sheria au amri ya kukamatwa.
Ninachoweza kusema hapa ni kuwa
kilichotokea kwa Profesa Lipumba tusikichukulie kivyama bali tuangalie
kwa upeo mpana wa kuendeleza amani na ushirikiano kati ya polisi na raia
na mali zao.
Namshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania, IGP Ernest Mangu na safu yake ya uongozi kwamba jeshi lake
liepuke kuonekana kana kwamba bado lina mfumo wa kikoloni ambao walikuwa
wakikandamiza raia kwani linafanya yale yale yaliyokuwa yakifanywa
wakati wa ukoloni.
Nizidi kukushauri IGP Mangu kuwa sheria
za polisi zibadilishwe kwa kuwa zina mfumo wa ukandamizaji na kwamba
ikibaki hivyo italiingiza taifa kwenye maafa makubwa na ni hatari polisi
kuwa adui wa raia wema.
Mwisho niwapongeze wabunge wote walioona athari ya kitendo kile hasa Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba ambaye alisema hata kama serikali inaundwa na CCM, lakini si kweli yanayofanywa na dola yote ni maagizo ya chama hicho.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Mwisho niwapongeze wabunge wote walioona athari ya kitendo kile hasa Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba ambaye alisema hata kama serikali inaundwa na CCM, lakini si kweli yanayofanywa na dola yote ni maagizo ya chama hicho.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
tiko
tiko
Post a Comment