tiko
tiko
Kwako Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Najua una taarifa juu ya kusambaa kwa video inayomuonesha mwanaume mmoja anayedai kuwa ni kiongozi wa kundi la wanaharakati wa kidini, Kais bin Abdullah aliyojirekodi akitoa vitisho vikali kwa jeshi la polisi, waziri mkuu, serikali na waumini wa dini tofauti na yake.
Najua una taarifa juu ya kusambaa kwa video inayomuonesha mwanaume mmoja anayedai kuwa ni kiongozi wa kundi la wanaharakati wa kidini, Kais bin Abdullah aliyojirekodi akitoa vitisho vikali kwa jeshi la polisi, waziri mkuu, serikali na waumini wa dini tofauti na yake.
Nilishawahi kuzungumza nawe siku za nyuma kwamba mwenendo wa jeshi la
polisi, unaonekana kulegalega sana na kwamba nguvu ya ziada ya kulisuka
upya inahitajika.
Leo sitapenda kuzungumzia hilo kwani tangu nilipozungumza nawe kupitia
ukurasa huu, matukio mengi yameendelea kutokea, yakiwemo ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi lako.
Yote tisa, kumi ni udhaifu mkubwa wa jeshi lako kushindwa kujilinda na matokeo yake kusababisha vituo vya polisi kuvamiwa, kutekwa kwa silaha zikiwemo bunduki na mabomu pamoja na baadhi ya askari kuuawa katika vitendo hivyo.
Yote tisa, kumi ni udhaifu mkubwa wa jeshi lako kushindwa kujilinda na matokeo yake kusababisha vituo vya polisi kuvamiwa, kutekwa kwa silaha zikiwemo bunduki na mabomu pamoja na baadhi ya askari kuuawa katika vitendo hivyo.
Vituo vya polisi Ikwiriri, Ushirombo na Tanga vimevamiwa na silaha
nyingi kuporwa na katika kipindi ambacho hakuna aliyekuwa anajua ni nani
aliyekuwa nyuma ya matukio hayo na silaha zilizokuwa zinatekwa zilikuwa
zinakwenda wapi, ndipo ilipoibuka video hiyo ikiwa na majibu ya maswali
ambayo wengi walikuwa wakijiuliza.
Kais bin Abdullah, anaeleza kwa ufasaha kabisa katika video hiyo kuwa,
wao ndiyo wanaohusika katika matukio hayo na kwamba wanakusanya silaha
kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi na wote waliohusika kwa
namna moja au nyingine, kuwakamata, kuwatesa na kuwafanyia vitendo vya
udhalilishaji mkubwa watu aliowataja kuwa ni wanaharakati.
Mtu huyo anasikika akikukosoa wewe Mangu, kwamba licha ya kutoa taarifa
kwamba jeshi lako limewakamata wote waliohusika na vitendo vya uvamizi
wa vituo vya polisi vilivyotajwa na kuzirudisha silaha zote zilizokuwa
zimeporwa, ukweli ni kwamba bado silaha hizo wanazo na wanapanga kufanya
mashambulizi ya kushtukiza maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba za ibada,
kushinikiza wenzao waachiwe.
Kais Abdullah anaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wanaipa serikali muda
mfupi kuhakikisha matakwa yao yanatekelezwa. Ni imani yangu kuwa matakwa
hayo unayafahamu kwa sababu mkanda huo wa video unao.
Kama umepata fursa ya kuisikia video hiyo, utaelewa ni kwa kiasi gani
Abdullah na wenzake wamedhamiria kufanya walichokisema. Huu ni mtihani
mkubwa kwako na jeshi lako ambao ni lazima uufaulu ili kuendelea kulinda
na kudumisha amani iliyopo.
Ningekuwa mimi ndiyo wewe, ningeutumia mtihani huu kujipima weledi na
ufanisi wangu katika kazi, nisingeacha Watanzania waendelee kutishiwa
amani na kikundi cha watu wachache wakati jeshi imara lipo.
Bila shaka hivi ni vitisho vya hali ya juu kabisa! Na huu ni wakati wako
sasa wa kuonesha kuwa wale wanaoamini kwamba kazi uliyopewa imekushinda
wanaaibika. Onesha umwamba wako kwa kupambana na kundi hili kabla
halijaleta madhara makubwa katika nchi yetu ambayo kwa kipindi kirefu
imekuwa ikijipambanua kama kisiwa cha amani.
Wasalaam!
Wasalaam!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment