tiko
tiko
MTU mmoja
mwanamume, aliyetajwa kwa jina la John Weghai amemjeruhi vibaya mke
wake, Anastazia John (18) kwa kumkatakata na mapanga kwa kile
kinachodaiwa kuchelewa kwake kupata ujauzito, katika maisha ya wawili
hao waliyoanza Februari mwaka jana.
Mwanamke, Anastazia John (18) anayedaiwa kucharangwa mapanga na mume wake, John Weghai.
Tukio hilo la kinyama lilitokea katika
Kijiji cha Mariba, Kata ya Mriba, wilayani Tarime mkoani Mara na
majeruhi huyo amelazwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji ambapo
ameshonwa nyuzi 67.Akizungumzia tukio hilo, msichana huyo alisema kuwa
mumewe amekuwa akimpa matatizo mengi katika ndoa yake kiasi cha
kumkosesha amani kwa kumpiga mara kwa mara akimtuhumu kuchelewa kupata
ujauzito.
“Kwa kweli nimekuwa nikipata mateso
makubwa tangu niishi na mwanaume huyu, nimekuwa nikipigwa mara kwa mara
sababu nachelewa kupata mimba na yeye anataka mtoto.
“Naviomba vyombo vinavyotetea na
kusaidia matatizo ya ukatili kama haya viweze kusaidia watu wanaofanyiwa
maana yanaondoa utu wa mtu na kumfanya kuishi kinyonge,”alisema
Anastazia.
Alisema siku hiyo alipata majeraha makubwa katika began a titi lake la kushoto, kitu kinachompatia maumivu makubwa.
Alisema siku hiyo alipata majeraha makubwa katika began a titi lake la kushoto, kitu kinachompatia maumivu makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Valeria Msoka, alisema
wamesikitishwa na tukio hilo, akisema ni ukatili uliopitiliza lakini
wataendelea na jitihada za kupambana na matukio ya namna hiyo katika
jamii.
Alisema muda mfupi tu umepita tokea
warejee kutoka wilayani Tarime wakiwa na ugeni mkubwa wa kimataifa
kupambana na masuala ya ukatili na kutoa ujumbe kwa wananchi juu ya
athari zake lakini kuna watu hawajabadilika.
“Tulitoa maoni kwenye Katiba mpya
inayopendekezwa na tunashukuru yamepita juu ya kuangaliwa upya kwa
sheria ya wanaofanya makosa ya ukatili kwenye jamii huenda ikaja kuwa
suluhisho juu ya matukio haya,”alisema Msoka.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi
Kanda maalum ya kipolisi Tarime/Rorya limesema mtuhumiwa bado
hajakamatwa na jitihada za kina zinaendelea kufanywa ili kuhakikisha
anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kaimu Kamanda wa Tarime/Rorya, Sweetbet
Njwewike alisema katika tukio hilo lililotokea Januari 22 mwaka huu
lilichelewa kutolewa taarifa jambo ambalo limechelewesha kupatikana kwa
mtuhumiwa.
Tukio hilo limetokea siku chache tu tokea mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Graca Machel kuwepo wilayani Tarime, akihamasisha kampeni ya kuepuka ukatili kwa watoto na akina mama.
Tukio hilo limetokea siku chache tu tokea mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Graca Machel kuwepo wilayani Tarime, akihamasisha kampeni ya kuepuka ukatili kwa watoto na akina mama.
tiko
tiko
Post a Comment