tiko
tiko
Huku zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya michuano ya AFCON kuanza wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Equatorial Guinea wamemfukuza kocha wao Andoni Goikoextea huku wakishindwa kutoa sababu za maamuzi haya .
Andoni amedukuzwa kazi baada ya uchaguzi wa shirikisho la soka la Equatorial Guinea kufanyika ambapo kazi ya kwanza iliyofanywa na uongozi mpya ilikuwa kumfukuza kazi kocha huyo Mhispania .
Rais mpya wa shikisho la soka Equatorial Guinea Andres Jorge Mbomio alithibitisha uamuzi wa kumfukuza Andoni Goikoextea ambaye amekaa na timu ya taifa hilo kwa miaka miwili na hakutaja sababu za msingi za kufukuzwa kwa nkocha huyo hali ambayo inatishia kuvuruga maandalizi ya wenyeji hawa wa Afcon kuelekea kwenye michuano yenyewe .
Hata hivyo inadaiwa kuwa kiwango duni ambacho Equatorial Guinea imekionyesha kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kikosi B cha klabu ya Benfica na Villafranquense huko nchini Ureno pamoja na kufanya vibaya kwenye michuano ya WAFU kumeufanya uongozi kukosa Imani naye japo muda uliobaki kuelekea kwenye AFCON.
tiko
tiko
Post a Comment