tiko
tiko
Vurugu zimetokea jana kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya makundi yanayopingana ndani ya Chama cha ACT-Tanzania kukutana ana kwa ana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kikao cha usuluhishi.
Baada
ya kukutana kwa makundi hayo, ghafla walitokea vijana wanaodaiwa
kukodiwa na Mwenyekiti aliyesimamishwa, Kidawi Limbuna kumvamia Katibu
Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson Mwigamba.
Vurugu
hizo zimetokea ikiwa ni siku chache baada ya Halmashauri Kuu ya chama
hicho kumsimamisha uongozi Limbu na kumwondoa katika nafasi yake
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
Mwigamba
alidai vijana hao wamekodiwa na Limbu kwa lengo la kumfanyia vurugu
baada ya kuona mikakati yake imekwama ndani ya chama.
“Limbu
alikuja na kundi la vijana kama 12, kati yao wawili aliwasafirisha kwa
ndege kutoka Arusha na mmoja anaitwa Gerald Emmanuel, pia alikuwamo
Mwenyekiti wa Geita, Katibu Uenezi Ukonga, Katibu Uenezi Jimbo la
Kinondoni pamoja na kina Mahona.
“Wakati
tunatoka kikaoni nikawa pale nje nasubiri gari linichukue, akaja Gerald
huku akishika shati langu akidai ananidai shilingi milioni moja na
lazima nimlipe pale pale, nilishangaa sana na hapo ndiyo nikajua kuna
kitu Limbu amefanya ili wale vijana wanivuruge na baadaye nikasirike na
kuonekana nimepigana,” alisema Mwigamba.
tiko
tiko
Post a Comment