tiko
tiko
HOMA ya
Uchaguzi Mkuu 2015 inazidi kupanda. Wapo baadhi ya wagombea wa urais
ambao tayari wameshatangaza nia hadharani lakini wengine wanaendeleza
harakati zao chini kwa chini.
Miongoni mwa makada ambao tayari wameonesha nia ya kutaka kugombea ni pamoja na vijana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (40) na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba (41).

Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba
Magharibi mkoani Singida, amekuwa na mvuto wa aina yake kisiasa huku
akionekana kupendwa zaidi kutokana na kujiwekea nembo yake kwenye mavazi
anayovaa kwa kujifunga skafu ya bendera ya taifa.
Mbali na mvuto, Mwigulu tayari
alishaanza mizunguko katika majimbo mbalimbali nchini na kuanza kupiga
kampeni za ‘kiaina’ ambapo ameonekana kukubalika katika maeneo
mbalimbali aliyopita ikiwemo Tanga na Morogoro kabla ya kupigwa ‘stop’
na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kuonesha kwamba amejipanga, Mwigulu
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alizua gumzo zaidi
alipokuwa akitumia usafiri wa helkopta katika ziara zake ambazo zilikuwa
zikitoa taswira kwamba kweli anakubalika na wengi.
Kwa upande wake Makamba, Mbunge wa
Bumbuli, alionesha nia mapema na kuwafanya vijana wengi wampe sapoti
katika harakati zake za urais.
Umaarufu wa Makamba pia unachagizwa
zaidi ya umaarufu na misimamo aliyokuwa nayo baba yake, aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa wa Dar na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ambaye alikuwa
akifanya mambo mengi ya maendeleo na kukemea matatizo mbalimbali nchini.
Mbali na mvuto wa uongozi, Makamba
amezua gumzo zaidi baada ya kutoa kitabu chake ambacho kinaelezea
mikakati ya kuwania nafasi ya urais.
Mwigulu na Makamba wanazua msuguano
mzito kutokana na kigezo cha ujana ambacho kinawabeba, hali ambayo
imewafanya wananchi wanaoamini katika falsafa ya viongozi vijana
kushindwa kupata jibu la moja kwa moja juu ya nani atapendeza kupitishwa
na chama.
Ukiachana na kigezo hicho, vijana hao ni
wasomi. Mwigulu ana ya Shahada ya Uzamili ya Uchumi, Shahada ya Uchumi
na Cheti cha Uongozi ambapo masomo yake amehitimu Chuo Kikuu cha Dar.
Makamba yeye ana Shahada ya Uzamili ya Diplomasia na Usuluhishi wa Migogoro, Shahada ya Diplomasia na Usuluhishi wa Migogoro ambazo amehitimishia katika Chuo cha George Mason, Marekani.
Makamba yeye ana Shahada ya Uzamili ya Diplomasia na Usuluhishi wa Migogoro, Shahada ya Diplomasia na Usuluhishi wa Migogoro ambazo amehitimishia katika Chuo cha George Mason, Marekani.
Wote wawili wana uzoefu mkubwa ndani ya
chama. Mwigulu kabla ya kuwa Naibu Waziri wa Fedha mwaka jana,
amekitumikia chama tangu hatua ya mkoa, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
na Umoja wa Vijana (UV-CCM) nafasi ambazo anazitumikia hadi sasa.
Makamba naye vivyo hivyo, ana uzoefu wa
kutosha chamani kuanzia ngazi ya afisa wa mambo ya nje chini ya Rais
Jakaya Kikwete ambaye pia alizunguka naye nchi nzima katika kampeni zake
mwaka 2005.
Swali la kwamba nani ataibuka kidedea kuwakilisha nafasi ya ugombea kupitia chama chao ndilo ambalo linaleta utata kutokana na sifa za kila mmoja, tusikilizie hadi Machi, mwaka huu pale atakapotangazwa rasmi.

Post a Comment