tiko
tiko
Mtoto
mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja, Yadiko Chigoda amelazwa katika
Hospitali ya Benjamini Mkapa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya
kupigwa na mchi kichwani na baba yake mzazi na kumsababishia maumivu
makali.
Akizungumza
na paparazi mama mzazi wa mtoto huyo, Carolina Mnyawami mkazi wa
Kijiji cha Mingui Kata ya Lumuma wilayani hapa alisema, tukio hilo
limetokea jana saa 4 asubuhi wakatimume wake Fabian Chigoda alipokuwa
akipigana na kaka yake kwa kuchapana fimbo na yeye aliamua kuwaamulia
ugomvi huo.
“Nilipowanyang’anya
fimbo ili wasiendelee kupigana, mume wangu aliokota mchi na kunirushia
kichwani... Niliukwepa ili usinipige ndipo ulipompiga kichwani mwanangu
niliyekuwa nimembeba mgongoni,” alisema Carolina.
Aliongeza kuwa, “Baada ya kuona kuwa amempiga mtoto alikimbia na hajulikani alipo mpaka sasa.”
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Said Mawji amethibitisha kumpokea mtoto huyo
na kwamba kwa sasa anaendelea kupatiwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
“Mtoto
huyo aliumia sana kichwani lakini bado tunampatia tiba na uchunguzi
zaidi kwenye fuvu la kichwa, kwani inaonekana kama vile limepasuka.”
Hata
hivyo, alisema wanafanya mpango wa kumpa rufaa mtoto huyo ili aweze
kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Mingui, Mwingwa Udoba alisema chanzo cha tukio
hilo ni ugomvi wa kifamilia na kwamba bado wanamtafuta baba mzazi wa
mtoto huyo kwa kuwa alikimbia baada ya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa simu yake ilipokewa na mtu aliyesema yuko kwenye kikao cha kazi.
tiko
tiko
Post a Comment