tiko
tiko
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kesho itawasha moto upya bungeni
wakati itakaposoma ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), ikitarajiwa kuibua kashfa tatu nzito ikiwamo ya
misamaha ya kodi.
Kashfa
nyingine zinazotarajiwa kuibuliwa kesho ni, ufisadi katika gharama za
ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya
Korosho.
Habari
zilizotufikia jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
zilisema kuwa, tayari kamati hiyo imepokea ripoti ya ukaguzi huo ambayo
inaonyesha ufisadi wa kutisha katika maeneo hayo matatu na mengineyo.
Masuala
hayo matatu pia yaliibuka wakati wa vikao vya kamati za Bunge
vilivyomalizika Dar es Salaam wiki iliyopita, huku bodi ya korosho
ikibanwa kuhusu nyumba yake aliyouziwa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM),
Silvestry Koka.
Kwa
mujibu wa habari hizo, ripoti hiyo inayoonyesha jinsi ufisadi wa
kutisha ulivyofanywa katika ujenzi wa jengo la (VIP Lounge) na Serikali
inadai ilitumia Sh12 bilioni kulijenga, lakini mthamini wa majengo ya
Serikali ameeleza kuwa jengo hilo lina thamani ya Sh3 bilioni.
Katika
suala la misamaha ya kodi, PAC imepokea taarifa kutoka kwa CAG
ikionyesha kuwa misamaha hiyo iliyokuwa imefikia Sh1.5 trilioni mpaka
Juni 2013, lakini baada ya mwaka moja misamaha hiyo imeongezeka hadi
Sh1.8 trilioni mpaka Juni 2014.
“Kwa
mwaka moja tu, misamaha ya kodi imeongezeka kwa zaidi ya Sh300 bilioni.
Kiasi hiki ni kama escrow fulani (Fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow,
Sh306 bilioni),” chanzo cha habari kilidokeza.
Katika
vikao vya kamati hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilieleza kuwa
misamaha ya kodi imepanda kutoka Sh1.4 trilioni mwaka 2012/13 hadi Sh1.8
trilioni mwaka 2013/14, chanzo kikiwa ni misamaha ya kodi katika miradi
mikubwa. Ilisema kati ya misamaha hiyo, Sh676 bilioni zinatokana na
misamaha ya kodi inayotokana na Ongezeko la Thamani (VAT) na kuwa hali
hiyo itapungua iwapo nchi itaanza kutumia Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT).
Pia,
TRA ilifafanua kuwa mpaka sasa wafanyabiashara na kampuni kubwa
zimefungua kesi katika mahakama ya rufaa wakipinga kulipa kodi ambayo
inafikia Sh1.7 trilioni.
Mvutano mwingine unaotarajiwa kuibuliwa katika ripoti hiyo ni uwasilishwaji wa utata wa uuzwaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.
Awali,
hati ya nyumba hiyo ilikuwa ya Taasisi ya Kilimo Tanzania ambayo
ilifutwa mwaka 1963, kabla ya mtu mwingine kuibadilisha hati na kuiuza
kwa Koka mwaka 2011.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mudhihir Mudhihir alisema Koka aliuziwa nyumba na taasisi hiyo ambayo haikuwa mmiliki halali.
Alisema
nyumba hiyo iliuzwa kwa Sh300 milioni na katika juhudi za bodi
kufuatilia taratibu za kuirudisha, ikagundulika kuwa hati
imeshabadilishwa, kusisitiza kuwa uuzwaji wa nyumba hiyo ulifanyika
kimakosa bila kufuata sheria na taratibu.
Juzi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikaririwa akiwataka
wananchi kutoa taarifa kuhusu makusudio ya kuuza nyumba za Serikali na
mashirika ya umma, kutokana na madeni mbalimbali ili ziweze kukombolewa
kabla ya kuuzwa.
tiko
tiko
Post a Comment