tiko
tiko
Leo
tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika
familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao
za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa
kupata watoto.
Kuna wengine wanapata watoto au mtoto
mmoja na baadaye wanashindwa kupata mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa
zinaharibika mara kwa mara.
Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba
asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika, najua watu wengi wanaweza
wakashangaa lakini ni kweli tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa
watu wengi huwa hawaelewi au wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba
zao zimeharibika kwani hutoka au huaribika kabla wao hawajagundua kama
walikuwa wajawazito.
Isipokuwa wale ambao hujua kwamba
walikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20,
na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba
zao zimeharibika au walikuwa wajawazito.
Kwa maana hiyo basi wewe ambaye
unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na umekuwa haupati lakini unakuwa
unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa mara kadhaa halafu hedhi inakaa
sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika
pasipo wewe kujua.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu
nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba, pale mwanamke anapopata
ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi
au kutokwa na damu katika via vyake vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe
mwanamke ambaye umepata ujauzito na bado unaona damu inatoka
kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo cha afya kabla tatizo
halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba (miscarriage) huwa hakutokei
ghafla tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii kutokwa na damu
ilihali wewe ni mjamzito.
Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa
na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito, na wakati mwingine
mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu nyepesi na kabla
hajatahamaki, damu ile nzito inaanza kutoka tena, na hii ni dalili mbaya
sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi na kuna uwezekano
ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na
dalili ile ya kwanza ni vema zaidi kufuata ushauri wa daktari ili
kuulinda ujauzito wako.
Dalili nyingine kubwa ni uchovu na
maumivu makali ya kiuno na mgongo, kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado
ni changa na unapatwa na maumivu makali sana ya mgongo au kiuno au vyote
kwa pamoja basi ni vema kuwahi kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi
gani unaweza kuzuia ujauzito wako usitoke au usikumbwe na tatizo hili la
kutokwa na ujauzito (miscarriage).
Kama unapatwa na dalili kama hizi
kutokwa na damu nyepesi au nzito ilihali wewe ni mjamzito basi ni vema
kuwahi kituo cha afya au wasiliana nasi ili kukusaidia.Kwa ushauri
vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam,
Tanga, Morogoro na Mwanza.
Nawatakia afya njema.
Nawatakia afya njema.
Itaendelea wiki ijayo!
tiko
tiko
Post a Comment