tiko
tiko
Miongoni mwa story zilizochukua headline Jan 2 ni kuhusu kikundi cha vijana wa ‘Panya Road’ kuvamia maeneo mbalimbali, kupora vitu na kupiga watu.
Mwaka jana msanii wa filamu, Kajala Masanja alizindua filamu mpya ‘Mbwa Mwitu‘ iliyotengenzewa chini ya kampuni yake ya Kajala Entertainment, kulikuwa na baadhi ya washiriki ambao ni vijana waliokuwa wakijihusisha na matukio ya uhalifu.
Akizungumza na kipindi cha Take One ya Clouds TV, Kajala amesema; “Ilikuwa
ni kazi ngumu sana kwani tuliwapa hela hata ya kutumia kidogo then
tukawaomba hayo vijana walikiri kweli walikuwa katika hayo makundi
maarufu kama Panya Road na Mbwa Mwitu basi tukawachukua tukaelekea nao
location kutengeneza filamu yangu mpya ‘Mbwa Mwitu’ ambayo niliizindua
mwaka jana Century Cinema, Mlimani City“, alisema Kajala.
Kwa upande wao washiriki ambao walikuwa
wahalifu wamesimulia namna ambavyo walikuwa wakifanya matukio na baadaye
wakaamua kuacha; “Katika maisha yetu
ya uwizi tukaanza kufa mmoja mmoja yaani kadri ya mtu alipokuwa
anazidi kufa mimi cheo kilikuwa kinazidi kupanda yaani akili inatanuka
na matukio ya uhalifu ulikuwa unaongezeka, tushafanya matukio mengi
tumeshatoka watoto wa watu sadaka wengi mpaka sasa hivi tumeshaepuka na
ishu hizo tunamshukuru Mungu;’walisema vijana hao“-.
Hii ndio Trailer ya filamu hiyo iitwayo ‘Mbwa Mwitu’ iliyochezwa na wasanii wa Bongo Fleva, Quick Rocka, Hemed PHD, Kajala Masanja na baadhi ya vijana ambao walikuwa wakihusika na matukio kadhaa wanaojulikana kama Mbwa Mwitu, Panya Road na makundi mengineyo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment