STAA wa
filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ amemshauri msanii mwenzake,
Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupigania kuolewa na mwandani wake, Nuhu
Mziwanda ambaye alimvisha pete ya uchumba siku chache zilizopita kwa
kuwa kitendo hicho kwa sasa kimeshazoeleka.
Staa wa muziki wa mduara Zuwena Mohammed ‘Shilole’akivikwa pete na mwandani wake, Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Sandra
alisema anafagilia sana mapenzi ya wawili hao kwani anaona wanaendana
pamoja na utofauti wa umri uliopo anamtaka Shilole ahakikishe anaolewa
haraka iwezekanavyo kwani hata mwanadada Wema Sepetu alivishwa pete ya
uchumba na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mpaka sasa
hawajafunga ndoa malengo yao yameishia njiani.
Post a Comment