tiko
tiko
BAADA ya
kudaiwa kulipwa fedha na kuingia mitini kwenye matamasha mbalimbali,
mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani)
amenaswa akitumbuiza jukwaani akiwa na ujauzito mkubwa.
Tukio hilo lililowashangaza watu wengi
lilitokea Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Ilongero jimbo la Singida
Kaskazini kulipokuwa na mkutano wa hadhara aliokuwa akiuhutubia Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Wakati wananchi wakimsubiri Nyalandu
ambaye pia ni mbunge wa Singida Kaskazini ahutubie, zilitangulia
burudani za hapa na pale ndipo baadaye alipopanda Rose akiwa na kitumbo
‘ndii’ na kusababisha minong’ono chini kwa chini.
“Mh! Jamani huyu ni Rose kweli au macho
yangu? Si angepumzika? Mbona tumbo tayari kubwa hivi, hata kama ni
kusaka pesa lakini si kwa staili hii, kuna wakati mtu inabidi fedha
uzipe kisogo,” alisikika mmoja wa wananchi.
Hata hivyo sambamba na watu kutilia
shaka juu ya afya yake, Rose alionekana kulimudu vyema jukwaa kwa
kutumbuiza nyimbo zake huku akiimba kwa staili ya kurukaruka kama
kawaida.
Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na
mamia ya wakazi wa Ilongero na jimbo zima la Singida Kaskazini, mbali na
kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, Nyalandu alitangaza nia ya
kugombea urais mwakani.
tiko
tiko
Post a Comment